MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, August 31, 2012

Ratiba ya Ligi Kuu

 
 
 
 



LIGI KUU TANZANIA BARA 2012/2013
Michuano ya Ligi Kuu kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013 itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.
 
Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).
 
Mzunguko wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).
 
Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.
 
MECHI YA UFUNGUZI WA MSIMU WA LIGI 2012/2013
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
SERENGETI BOYS KUJIPIMA KWA ASHANTI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyokuwa kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya itavunja rasmi kambi yake kesho (Jumamosi) kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United.
 
Mechi hiyo dhidi ya Ashanti United iliyoko daraja la kwanza itachezwa kuanzia saa 10 jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 2,000.
 
Serengeti Boys ilikuwa Septemba 9 mwaka huu icheze na Kenya kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini Kenya ikajitoa ambapo sasa itacheza na Misri katika raundi ya pili. Mechi ya kwanza itachezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 
Mwishoni mwa Septemba, Serengeti Boys itarejea tena kambini kujiandaa kuikabili Misri ambapo kabla inatarajia kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu itakayotangazwa baadaye.
 
MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR NAYE APATA ITC
Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull FC ya nchini humo.
 
ITC hiyo ilitumwa jana (Agosti 30 mwaka huu), hivyo kufanya wachezaji ambao ITC hazijapatikana hadi sasa kubaki wawili tu. Dirisha la usajili wa wachezaji litafungwa rasmi Septemba 4 mwaka huu.
 
Wachezaji ambao ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC Leopards ya Kenya waliojiunga na Simba. ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati wowote kwani tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshaziomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa zikitakiwa kupatikana.

Thursday, August 30, 2012

Hatimaye Mbuyu Twite atua

Beki mpya wa timu ya Yanga, Mbuyu Twite akiwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, jana kwa ajili ya Ligi Kuu kwa mwaka 2012/13

Dk. Salmin atunukiwa Udaktari wa heshima

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Profesa. Idris Ahmada Rai (kushoto) akimkabidhi Shahada ya uzamivu (PHD)  ya heshima ya Chuo Kikuu hichoc, Rais mstaafu wa awamu ya tano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour Juma nyumbani kwake Migombani mjini Zanzibar. Kulia ni mjumbe wa Baraza, Mohammed Said Dimwa

Wednesday, August 29, 2012

ziara Mbunge wa Mvemero ambaye pia ni Naibu Waziri, Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makalla

 Mbunge wa Mvomero ambaye pia ni Naibu Waziri, Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Kunke na Kidudwe kata ya Mtibwa wakati wa ziara katika jimbo hilo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na kuwasilikiliza kero zao, ambapo aliweza kukabidhi Mifuko 200 ya Saruji  kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Zahanati katika vijiji hivyo na kukabidhi Pikipiki sita  kwa kata sita kwa ajili ya Shughuri za kila siku za Chama cha Mapinduzi
 Mbunge wa Mvemero na Naibu Waziri, Amos Makala akiwahutubia wananchi wa Kidwe na Kunke
 Mbunge wa Jimbo la Mvemero (CCM) na pia Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akimkabidhi Pikipiki Moja wa Makatibu watendaji wa Kata

 Mbunge wa Mvemero, Amos Makala akimkabidhi vifaa vya Ofisini Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Wilaya Mvemero, Pololet Mgema baada ya kufanya Mkutano na wananchi wa Kijiji cha Kidudwe kata ya Mtibwa hivi karibuni
 Mbunge wa Mvomero, Amos Makala akikagua Kivuko kinatumiwa na wakazi wa Kijiji cha Kisala kabla ya kufanya Mkutano na wananchi akiwa katika ziara katika Jjimbo hilo hivi karibuni
Mbunge wa Mvomero, Amos Makala akikagua Kivuko kinatumiwa na wakazi wa Kijiji cha Kisala kabla ya kufanya Mkutano na wananchi akiwa katika ziara katika Jjimbo hilo hivi karibuni
 Mbunge wa Mvemero, Amos Makalaa akikagua Ujenzi wa Daraja katika Kijiji cha Kisala
 Nahodha wa timu ya Sasa Kazi FC ya Kijiji cha Kisala kata ya Mtibwa mkoani Morogoro, Rashid Sumuri akifurahi baada ya kukabidhiwa jezi na Mpira kwa ajili ta timu hiyo na  Mbunge wa Mvemeroi, AMos Makalla . Pia aikabidhi mpira wa Pete kwa ya Netiball na vijana chini ya umri wa miaka 17
 Mbunge wa Mvemero na Naibu Waziri, Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makala akikagua Gwaride wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Polisi Jamii na Ulinzi Shiriki katika Kata ya Sungaji ikiwa ni Mwendelezo wa ziara ya kutembelea jimbo la Mvomero, Jumla Vijana 400 walimaliza mafunzo hayo na pia kuahidi kuwa Mlezi wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi
 Mbunge wa Mvemero na Naibu Waziri, Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akijiandaa kukabidhi Mifuko 70 ya Saruji kwa Mwalimu Kiongozi wa Shule ya Msingi Mkindo B kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika Shule hiyo

Saturday, August 25, 2012

Shirika la Hope Foundation Club washiriki katika Kampeni ya Usafi Bagamoyo

 Baadhi ya watoto wanaohudumiwa na Shirika la Hope Foundation Club wakishiriki katika Kampeni ya kusafisha mji wa Bagamoyo mkoani Pwani leo
 wakiokota uchafu kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi Bagamoyo
 Wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Hope Foundation Club, Princess Marsland
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Hope Foundation Club, Princess Marsland linalowahudumia baadhi ya watoto yatima, walioathirika na wanaoishi katika Mazingira magumu akiwaongoza watoto hao kuokota takataka wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuusafisha mji wa kihistoria wa Bagamoyo
 Vijana wakiokota takataka eneo la Ufukwe wa Bahari ya Hindi Bagamoyo
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Hope Foundation, Princess MarslandClub akiwaelekeza jambo vijana wanaohudumiwa na Shirika hilo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Hope Foundation Club , Princess Marsland akisaidiana na vijana hao kufanya usafi

Friday, August 24, 2012

Dar es Salaam yazidi kubadilika kila siku

Hili ni jengo la NHC HOUSE lillilopo katika Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi

Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) yazinduzi wa Mpango Kasi wa Uwezeshaji wanawake

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Salma Kikwete (katikati) akiwa katika hafala ya kuzindua Mpango Kasi wa Uwezeshaji  wanawake na wasichana uliofanyika, Dar es Salaam leo
 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Salma Kikwete (kulia) akiwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakati wa uzinduzi wa Mpango Kasi wa Uwezeshaji  wanawake na wasichana,   uliofanyika leo Dar es Salaam

kamati Kuu ya CCM


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu cha CCM jana 24, Dar es salaam. Picha na Ikulu.

SENSA

Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Paul Chagonja, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam jana, kuhusu jinsi walivyojipanga kuhakikisha zoezi la sensa linafanyika katika hali ya utulivu na amani

Thursday, August 16, 2012

CHADEMA KUFUNGUA TAWI MAREKANI

UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA JIJINI HUSTON TX.
Tunapenda kutoa habari hizi kwa waTanzania wote na wapenda maendeleo, Siku ya Jumamosi Aug 25 kutakuwa na ufunguzi rasmi wa tawi la chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Jijini Houston Texas Nchini Marekani, Wageni rasmi wa ufunguzi wa tawi hilo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Jodeph Mbilinyi (Mr. 2/Sugu) Sherehe za ufunguzi wa tawi hilo zitaanza mida ya saa 5:PM (Jioni)

Wednesday, August 15, 2012

Taifa Stars na Botswana

Taifa Stars imetoka sare ya mabao 3-3 na wenyeji Botswana (Zebras) katika moja kati ya mechi kadhaa za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zilizochezwa leo (Agosti 15 mwaka huu) usiku.
 
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Molepolole ulioko Kilometa 40 nje ya Jiji la Gaborone, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa kwa penalti na beki Erasto Nyoni.
 
Mwamuzi Lekgotia Johannes Stars alitoa adhabu hiyo baada ya beki Oscar Obuile Ncenga wa Zebras kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akimkabili kipa Mompoloki Sephekolo.
 
Bao hilo halikudumu muda mrefu, kwani Zebras walisawazisha dakika ya 26 baada ya shuti kali lililopigwa na Lemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja. Dakika tano baadaye kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars bao la pili kwa shuti la mbali.
 
Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37. Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto uliopigwa na Tebogo Sembowa ambaye kabla alimtoka beki Aggrey Morris.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa Kocha Kim Poulsen wa Stars kuwatoa Frank Domayo na Salum Abubakar na nafasi zao kuchukuliwa na Shabani Nditi na Athuman Idd. Safari hii Zebras ndiyo walioanza kufunga dakika ya 69 ambapo kiungo Michael Mogaladi aliifungia bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi fupi iliyotokana na mpira wa kurusha.
 
Dakika 13 za mwisho Stars walicheza pungufu baada ya beki Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu mshambuliaji Lovemore Murirwa.
 
Mrisho Ngasa ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo aliisawazishia Stars dakika ya 84 baada ya kugongeana one-two na mshambuliaji Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Moshi.
 
"Licha ya timu kucheza vizuri, tatizo kubwa lilikuwa kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki waliruhusu mipira mingi ya krosi na kuwaacha washambuliaji wa Botswana wakifunga bila bughudha. Mabeki hawatakiwi kuruhusu mipira ya krosi, wakiruhusu ni lazima wahakikishe wanawadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
 
"Kwa upande wa washambuliaji, Said Bahanuzi alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars tangu nilipomjumuisha kwenye timu kwa mara ya kwanza. Kuna makosa madogo madogo ambayo niliyatarajia, hivyo nitamrekebisha polepole," alisema Kocha Poulsen mara baada ya mechi hiyo.
 
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo/Shabani Nditi, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar/Athuman Idd, Said Bahanuzi/Simon Msuva, Haruna Moshi/Ramadhan Singano na Mwinyi Kazimoto.
 
Zebras; Mompoloki Sephekolo, Tshepo Motlhabankwe/Tshepo Maikano, Edwin Olerile, Oscar Obuile Ncenganye, Mompati Thuma, Patrick Motsepe/Jackie Mothatego, Lemponye Tshireletso, Michael Mogaladi, Tebogo Sembowa, Ntesang Simanyana na Galabgwe Moyana/Lovemore Murirwa.
 
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inarejea nyumbani kesho (Agosti 16 mwaka huu) ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.