MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, August 25, 2013

WACHEZAJI WA SIMBA WAPATA HATI ZA UHAMISHO (ICT)

MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, leo mchana amefanikisha upatikanaji wa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa wachezaji wawili wa klabu hiyo kutoka nchini Burundi -Amissi Tambwe na Gilbert Kaze.

Wachezaji hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya taifa ya Burundi (Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania iliyochezwa jana kutokana na kutokamlika kwa uhamisho huo, jambo lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji wenyewe, uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu.


Rage aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku na imechukua chini ya saa 24 kuweka kufanikisha suala hilo. Katika taarifa yake kwa wana Simba, Mbunge huyo wa Tabora Mjini alisema amelazimika kuingilia kati suala hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa Vitalo, klabu waliyotoka wachezaji hao hawakuwa mjni na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba.


"Kila walipokuwa wakipigiwa simu kwa takribani siku tatu mfululizo walikuwa wakisema kwamba wako milimani. Sasa hawa watu wa Burundi wakikwambia wako miliman wanamaanisha wameenda kijijini kwao. Kuongea kwa simu pekee kusingetosha na ndiyo Kamati ya Utendaji ya Simba iliomba niende mwenyewe Burundi ili suala hili liishe," alisema.


Hii ni mara ya pili kwa Rage, ambaye ana uzoefu wa kuongoza soka kwa zaidi ya miongo mitatu, kuingilia kati suala la uhamisho wa wachezaji wa kimataifa. Miaka miwili iliyopita, Mwenyekiti huyo alilazimika pia kusafiri kwenda nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kushughulikia uhamisho wa mchezaji Gervais Kago ambao nao ulikuwa na matatizo.


Kutokana na kupatikana kwa ITC hizo, Kaze na Tambwe sasa wataruhusiwa kucheza katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya JKT OIljoro ya Arusha iliyopangwa kufanyika Jumatano ijayo mjini Arusha. Klabu ya Simba tayari imewakatia wachezaji hao vibali vya kufanya kazi hapa nchini.


Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba, Joeph Owino na Abel Dhaira, walicheza katika mechi ya jana kutokana na kukamilisha taratibu zote za uhamisho na kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini.


Imetolea na


Ezekiel Kamwaga

Ofisa Habari
Simba SC

Friday, August 23, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU NA NAIBU MAKATIBU WAKUU IKULU DAR ES SALAAM

Baadhi ya makatibu wakuu na Naibu makatibu wakuu wakipitia viapo vyao kabla ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo
 Picha ya pamoja ya Mawaziri, Makatibu Wakuu walioapishwa na Naibu Makatibu wakuu wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuapishwa
Dr. Deodatus Michael Mtasiwa na familia yake baada ya kuapishwa
Rais Jakaya Kikwete (katikati), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali, Davis Mwamunyange, Mkewe, Monica Mwamunyange wa tatu kutoka (kushoto) aliyeapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja

MAJINA YA WAOMBAJI UONGOZI TFF, TPL BOARD YAWEKWA WAZI

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebandika rasmi kwenye ubao wa matangazo majina ya waombaji uongozi kwenye uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ili kutoa fursa kwa pingamizi.

Kipindi cha pingamizi kinaanza kesho (Agosti 24 mwaka huu) hadi sas 10 kamili jioni ya Agosti 26 mwaka huu ambapo waweka pingamizi wanaruhusiwa kupitia taarifa za wale wanaokusudia kuwawekea pingamizi kabla ya kuwasilisha pingamizi husika.

Kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi, Agosti 27 hadi 29 mwaka huu ni wawekaji pingamizi na wawekewa pingamizi kufika mbele ya Kamati ya Uchaguzi kwa ajili ya kusikiliza pingamizi.

Waombaji kuwania uongozi katika TFF ambao majina yao yamebandikwa ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard J. Rukambura (urais). Nafasi ya Makamu wa Rais ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Walace John Karia.

Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda ni Kanda Namba Moja (Kagera na Geita) ni Abdallah Hussein Mussa na Kaliro Samson. Kanda Namba Mbili (Mara na Mwanza) ni Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Kalwizira Lufano.

Kanda Namba Tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko na Stanslaus Haroon Nyongo. Kanda Namba Nne (Arusha na Manyara) ni Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii Ali.

Kanda Namba Tano (Kigoma na Tabora) ni Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamisi Kitumbo. Kanda Namba Sita (Katavi na Rukwa) ni Ayoub Nyaulingo, Blassy Mghube Kiondo, Nazarius A.M. Kilungeja. Kanda Namba Saba (Iringa na Mbeya) ni Ayoub Shaibu Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Samson Lugenge, Elias Lusekelo Mwanjala, Eliud Peter Mvella na John Mwachendang’ombe Kiteve.

Waombaji wa Kanda Namba Nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge. Kanda Namba Tisa (Lindi na Mtwara) ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder.

Kanda Namba Kumi (Dodoma na Singida) ni Charles Komba, Hussein Zuberi Mwamba na Stewart Ernest Masima. Kanda Namba 11 (Morogoro na Pwani) ni Farid Salum Mbarak, Geoffrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala na Twahil Twaha Njoki.

Wanaowania kuteuliwa kugombea kupitia Kanda Namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed wakati Kanda Namba 13 (Dar es Salaam) ni Alex Chrispine Kamuzelya, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.

Kwa upande wa TPL Board waliotangazwa kuomba kuwania uongozi wa juu ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).

Wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.

Thursday, August 22, 2013

Twanga Pepeta,Roma Mkatoliki kupamba Tamasha la wafanya mazoezi la Vita Malt jumamosi



Mkufunzi wa kimataifa wa maswa ya mazoezi ya viungo bwana SAAS akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya tamasha kubwa linalowakutanisha wafanya mazoezi kote nchini na familia zao linalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar Es Salaa ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kujumuika pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja sambamba na hilo pia burudani toka kwa bendi ya Twanga pepeta na Roma Mkatoliki na baa za kisuma na Fyatanga zitakuwepo kuchoma nyama kwa kipindi chote,Katikakati ni Meneja wa Vitamalt Plus Consolata Adam na Meneja mawasiliano na mahusiano wa Tbl Edith Mushi

 KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi na litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Consolata Adam alisema, wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuwakutanisha pamoja wafanya mazoezi wote, ambao mara nyingi wanafanyia katika vituo maalumu (gym).

Consolata alisema, bonanza hilo la aina yake kwa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama kuanzia saa 12 asubuhi hapo kesho (Jumamosi).

“Tumeamua kuandaa bonanza linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.

“Siku hiyo katika Viwanja vya Posta kutakuwa na gym kumi na mbili zilizo maarufu ambazo zitashiriki na kutakuwa na wakufunzi kumi ambao wataongozwa na mkufunzi wa kimataifa SAAS,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.

Alisema, lengo kuu kuu la bonanza  ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga umoja imara wa gym zilizopo nchini.

Consolata alisema, katika kuhakikisha bonanza hilo linakuwa bora na la kufana jumla ya gym kumi na mbili zitashiriki ambazo ni Better Life, Genessis ya Kijitonyama, Segerea Gym, Rio Gym,Genessis ya Kimara, Azula ya Mikocheni na Serena Gym.

Alisema pia baa zilizoshinda katika kuchoma nyama katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni za Fyatanga ya Tegeta na Kisuma Bar ya Temeke, zitaonyeshana umwamba kwa kuchoma nyama bomba kwa kipindi chote hicho.

“Tumeweka burudani za kila aina kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, Sehemu za watoto kuchezea pia na zawadi nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.”

NaYe Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi alisema mbali na hayo kutakuwa na burudani mbalimbali toka kwa bendi African Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii mkali wa Hip hop, Roma Mkatoliki sambamba na burudani nyingine nyingi kwa kipindi chote cha tamasha.

“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao siku ya Jumamosi, hakutakuwa na kiingilio chochote na vinywaji vyote toka TBL vitakuwepo.

“Lakini pia watu wa kawaida na wa rika zote siku hiyo hakutakuwa na kikwazo chochote cha kufanya mazoezi, kwani ni bure kabisa, hivyo nawashauri tufike kwa pamoja ili tuweze kupata pia ushauri mbalimbali juu ya kupunguza uzito na aina ya mazoezi yanayotakiwa,” alisema.

Vita Malt ni kinyaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Friday, August 9, 2013

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAHIMIZWA KUENDELEA NA MATENDO MEMA WALIYOKUWA WANAYANFANYA KIPINDI CHA MFUNGO WA MWEZI MTUKU WA RAMADHANI


Baadhi ya waumini wa Dini ya kiislamu wakishiriki swala ya idd el Fitri iliyoswaliwa kimkoa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.     
 Waumini wa Dini ya Kiisilamu  mkoani Dar es Salaam wakiswali katika viwanja vya Mnazi Momoja Dar es Salaam
 wakiomba dua

Sehemu ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliojitokeza kuhudhuria Swala ya Sikukuu ya Iddi, iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora leo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Shaaban Bin Simba, mara baada ya Swala ya Iddi iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora leo

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Mussa Salum, Mwenyekiti wa CU, Profesa Ibrahim Lipumba wakishiriki swala ya idd el fitri katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu mkoani Dar es Salaam wakishiriki swala ya Idd el Fitri

Wednesday, August 7, 2013

MRISHO NGASSA AANZA MAZOEZI YANGA

Mrisho Ngassa aliyesajiliwa na yanga akitokea timu ya simba alikokuwa anachezea kwa mkopo akitokea AZAM FC, hatimaye leo ameanza mazoezi na timu yake mpya ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajia kuanza mwezi ujao

MIFEREJI YA KUPITISHIA MAJI MACHAFU YAGEUZWA YA KUTUPIA TAKA

Mwanafunzi akiruka mtaro wa  kupitishia maji machafu eneoa la Tegeta Nyuki Dar es Salaam , hata hivo mifereji hiyo maeneo mengi imegeuzwa kuwa mifereji ya kutupia taka kama inavyooneka

KAMPUNI YA tIGO YAZIDI KUTOA BAJAJI

Bajaji saba zilizokabidhiwa kwa washindi walioshinda kwenye promosheni ya Miliki Biashara yako inayoendeshwa na Kampuni hiyo zikiwa kwenye viwanja vya Tegeta Nyiki jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa.
wasani wa kikundi cha Four Boys acrobatic wakiburudisha wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Bajaji kwa washindi wa Promosheni ya Miliki Biashara yako
 wasani wa kikundi cha Sarakasi cha Four Boys acrobatic wakiburudisha wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Bajaji kwa washindi wa Promosheni ya Miliki Biashara yako.
 Msanii wa kikundi cha Sarakasi cha Four Boys acrobatic wakiburudisha wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Bajaji kwa washindi wa Promosheni ya Miliki Biashara yako.

Tuesday, August 6, 2013

USAJILI WA WACHEZAJI HATUA YA KWANZA WAMALIZIKA


Hatua ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 imefungwa rasmi jana (Agosti 5 mwaka huu) ambapo klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao ndani ya wakati.

Baadhi ya klabu zimefanya makosa madogo madogo katika usajili ambapo zimepewa siku ya leo (Agosti 6 mwaka huu) kufanyia marekebisho kasoro hizo. Hivyo kesho (Agosti 7 mwaka huu) majina ya vikosi vyote yatabandikwa kwenye mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kipindi cha pingamizi kitakachomalizika Agosti 12 mwaka huu.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 14 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania. Hivyo, dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.