MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, September 19, 2014

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA KUANZA KUTIMUA VUMBI MWISHONI MWA WIKI HII

Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2014/15 kuanza kutimu vumbi mwishoni mwa wiki hii kwa vilabu 14 kumenyana katika viwanja tofauti.
Kila Klabu imejianda vya kutosha kwa ajili ya kukabiliana na timu pinzania kwa ajili ya kupata ushindi wa kujiweka katika hatua nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi Kuu inayodhaminiwa na Kampuni ya Simu ya mkononi, Vodacom Tanzania
Msimu uliopita timu ya Azam FC iliweza kuchukuwa ubingwa na kufuatiwa na Yanga na Mbeya City kushika nafasi ya tatu na Simba iliyoambulia nafasi ya nne.
Azam na Yanga zitashiriki katika michuano ya Afrika, huku Azam FC wakishirikia katika michuano mikubwa ya Klabu Bingwa Afrika na Yanga wakishiriki Kombe la Shirikisho.
Tumeona katika Ngao ya Jamii Yanga walivyowafunga, Azam FC goli 3-0 mabao mawili yakiwa yamefungwa na mshambuliaji kutoka Brazil aliyesajiliwa msimu huu maarufu kwa jina la JAJA.
Lakini Azam pamoja na kufungwa wao walisema hiyo haiwatishi kwamba eti wavunjike moyo kwamba hawataweza kuutetea ubingwa wao hicho siyo kigezo, akizungumza kocha msaidizi, Kally Ongara, alisema kufungwa ni sehemu ya mchezo Yanga wamewafunga na wameona wapi pa kurekebisha
 Michezo ya ufunguzi itakuwa kati ya Yanga na Mtibwa, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Azam wakimenyana na timu iliyopanda daraja msimu huu ya Polisi Morogoro kutoka mkoani Morogoro na Simba wao watashuka katika Uwanja wa Taifa kumenyana na wagosi wa Kaya siku ya Jumapili

No comments:

Post a Comment