MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Saturday, October 25, 2014

HATIMAYE JAJA AANZA KUZIFUMANIA NYAVU KATIKA MICHEZO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

Al maarufa Jaja , mshambuliaji wa kimataifa kutoka Brazil, hatimaye baada ya kuwika katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya wanalambalamba, Azam FC kwa kufunga mabao mawili dhidi ya matatu na kushindwa kuzifumania nyavu kwenye michezo minne ya Ligi kuu iliyochezwa, leo ameweza kuifungia timu yake ya yanga goli la kwanza katika dakika ya 13 dhidi ya timu mpya Stand United katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kamabarage mkoani Shinyanga, na timu ya Jangwani kuibuka na ushindi wa goli tatu kwa bila magoli mawili yakiwa yamefungwa na Jeryson Tegete, aliyetokea benchi. hivyo imeweza kufikisha pointi kumi kwa michezo mitano iliyokwisha cheza. Na huko Mbeya katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine, timu ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons imeendelea jinamizi la sare ikiwa ni sare ya tano katika michezo mitano iliyokwishacheza mpaka sasa, katika mchezo huo, simba iliandika bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji, Emmanuel Okwi aliyepiga mpira wa adhabu na kuzaa goli katika dakika ya tano, na Tanzania Prison wakasawazisha katika dk za lala salama, naye Mwenyekiti wa Usajili ya timu ya Simba, Hans Pope, akihojiwa  katika kipindi cha michezo cha Radio ya EFM alisema hafurahishwi na uchezaji wa Amri Kiemba ambaye anakuwa ndiye nguzo katikati, pindi anapocheza timu inapwaya  na kuruhusu goli, aliongeza kusema mbona akiwa kwenye timu ya Taifa anacheza kwa bidii lakini anashangazwa akiwepo katika klabu ya Simba, ameshauri kocha asimzoee kumpanga mara kwa mara maana, katika mchezo mingine , Azam FC imekubaili kwata za Ruvu Shooting kwa goli moja , Kagera Sugar imetoka sare ya moja , moja na Coast Union , mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera

No comments:

Post a Comment