MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Saturday, November 1, 2014

AZAM FC NA YANGA ZAFUNGWA KATIKA MFULULIZO WA MICHEZO YA LIGI KUU TANZANIA

 kikosi cha Yanga
Kikosi cha Azam FC.
Katika mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara,  iliyochezwa  katika viwanja tofauti hapa nchini, Yanga imejikuta ikizama kwa gori moja katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera dhidi ya Kagera Sugar, nao Azam FC wamejikuta wakichezea kichapo kutoka kwa timu ngeni iliyopanda daraja msimu huu ya Ndanda FC wanakuchele baada ya kukubali kufungwa goli moja bila majibu na huko katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, wazee wa sare, Simba Sports Club wamejikuta wakifikisha, Pointi Sita, Magoli ya kufungwa sita, magoli ya kufunga sita ukiwa ni mchezo wa sita dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kutoka Sare ya goli moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment