MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, July 1, 2012

Onesho la Supa 5 ya Airtel lilivyofana Mtwara

Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Amina Keita  (kushoto)akitoa zawadi ya simu kwa mmoja wa wakazi wa Mtwara, Nasra Salehewakati wa uzinduzi wa huduma ya  Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa
Mashujaa mjini Mtwara jana. Tukio hilo liliambatana na burudani kutokakwa wasanii chipukizi wa mkoani humo na baadhi ya wasanii maarufu kutoka katika Jiji la Dar es Salaam ambako waliohudhuria walielezwa
jinsi ya kujiunga na faida mbalimbali zinazopatikana katika huduma ya Supa 5.


Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akihutubia wakati  akizindua huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT, Mwansiti Almasiakikonga nyoyo za wakazi wa Mtwara waliohudhuria  uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani  Mtwara jana
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akitoazawadi ya simu kwa Jamimu Mohamed baada ya kuibuka mshindi kwa kutoa maelezo sahihi ya jinsi ya kujiunga na faida za huduma ya Supa 5 ya
Airtel wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana.


Msanii mkali wa miondoko ya  bongo flava, Juma Kassim Nature ‘Sir Nature’ kutoka kundi la Wanaume Halisi, akifanya vitu vyake  wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa
Mkoani  Mtwara jana

Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Mtwara na viunga vyake wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini humo jana
Mabinti  wa Mtwara wakichuana ili kumpata mshindi wa kusakata‘Kiduku’ ambapo mshindi wake, Nasra Salehe (kushoto) alijishindia simu katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel Mkoani Mtwara

No comments:

Post a Comment