
Rais
Kikwete, akiwa ameongozana na mke wake, Mama Salma Kikwete, pamoja na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa
Ghasia, aliwatembelea na kuwapa pole majeruhi Mohamed Ally Dhamji, Baqir Virani,
Selemani Saidi na Yusuf Abdallah waliolazwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
Majeruhi
hao, ambao kwa mujibu wa Daktari C.N. Mcharo wanaendelea vyema na matibabu na
hali zao ni za kuridhisha, ni wanne na kati ya sita waliolazwa katika taasisi
hiyo, ambapo wawili wamekwisharuhusiwa.
No comments:
Post a Comment