Pages
▼
Friday, August 3, 2012
Maonyesho ya Nanenane Dodoma
Afisa
Uhusiano wa Chuo cha Mipango Dodoma, Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha, Yulis Otto
(kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo
alioptembelea Banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Zuguni
mjini Dodoma.
Kaimu Afisa Uhusiano wa Mfuko wa
Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF), Hawa Kikeke (kushoto) na Afisa Malipo ya
Pesheni wa Mfuko huo kwa watumishi wa umma (PSPF), Andrew Dayson (wa pili
kutoka kushoto) wakiwasaidia Maafisa wa
Jeshi la Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia
tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea Banda la Wizara ya
Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Zuguni mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment