Kufuatia kufunguliwa kwa shule za Sekondari na za msingi, jana wasafiri walikuwa wengi sana waliokuwa wanatarajia kusafiri kwa mabasi kwenda mikoani, mabasi hayo kuonekana ni machache na kulazimu mabasi ya Daladala kuamua kuchukua abiria kuwasafirisha kwenda mfano ni mikoa ya karibu kama Tanaga
Baadhi ya abria wakisubiri usafiri baada ya kutopata basi takribani saa tano wakiwa eneo la Kituo Kikuu cha mabasi ubungo, Dar es Salaam
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Kilakala mkoani Morogoro wakisubiri usafiri eneo la Kituo Kikuu cha mabasi Ubungo Dar es Salaam.
Hapa wakiwa hawajui la kufanya baada ya kukaa zaidi ya saa sita bila mafanikio yoyote
Abiria waliokuwa wanasafiri kwenda mkoani Morogoro wakiwa wamelizunguka basi la Kampuni ya Abood ili kuweza kubahatisha kama wanaweza kupata nafasi ya kusafiri
No comments:
Post a Comment