Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam, wakiwa katika maandamano ya kupinga vitendo wanavyofanyiwa vya uzalilishaji na vibaka wa eneo la Kigamboni la kunyanga'nywa vitu ikiwa ni pamoja na Laptop na vitu vingine, waliamua kuandamana kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani kutokana na taarifa zao kupuuzwa na jeshi la Polisi Kituo cha Kigamboni ambazo wameshazifikisha kituoni hapo bila kutatuliwa. baada ya kufika Wizarani waliamuliwa waende kigamboni lilikotokea tatizo ili wakalimalizie huko
Hapa wakiwa eneo la geti la Feri ambapo waliingia bila kulipia
Askari wakilinda kituo cha Polisi cha Kigamboni baada ya wanafunzi hao kukata kuzungumzia swala lao katika Uwanja wa Machava kama walivyokubaliana na afande Kova
Baada ya wanafunzi hao kutaka kuingia kwa nguvu kituoni hapo ndipo askari walianza kujihami kwa kuwatawanya kwa mabomu ya machozi
Mmoa wa wanafunzi aliyekamatwa katika mkasa huo akipandishwa kwenye gari
Huyu akipelekwa kwenye gari baada ya kufanikiwa kukamatwa na askari
Twende kaka tumeshakukamata maana nyie hamtaki kusikia mnaloambiwa
Mmoja wa wanafunzi hao akiwa amelala chini baada ya kuanguka katika msako huo
Hapa ndipo walipokuwa wamejificha muda mfupi baada ya kukamatwa
Mikono juu ndivyo askari anavyowaambia hao wanafunzi baada ya kukamatwa
Ongozeni Kituoni baada ya kukamatwa sehemu waliokuwa wajificha wakati wa mabomu ya machozi yakipigwa
Nasema kaa chini kijana usilete jeuri hapa
Na wewe unaandamaa ebu kula lungu moja ujisikie
Hapa hakuna atakayetoroka vijana mmekwama
Panda humo hata kama huna viatu
Jamani mi nimezidiwa niacheni nasikia kizunguzungu
Jamani natii amri sirudii tena
Kule ruka kichura mpaka kituoni
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM, Michael Charle akizungumza na waandishi wa habari
Jamani mmenielewa ndivyo alivyokuwa anawaambia Kamanda wa Kanda Maalum, Suleimani Kova
No comments:
Post a Comment