Waziri wa Fedha Dk. Wiliam Mgimwa, amewaeleza Benki ya Dunia pamoja na Shirika la
Fedha la Kimataifa vipimo vya ukuaji wa nchi yetu kiuchumi ambapo unakuwa kwa
asilimia 6.9. Ukuaji huu wa uchumi ni mkubwa ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka uliopita 2011 ambapo ilikuwa ni asilimia
6.3.
Akizungumzia
mfumuko wa bei, Mgimwa alisema kuwa, mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 19.8 kwa Desemba mwaka 2011 na
kufikia asilimia 9.8 kwa mwezi Machi mwaka huu 2013. Aidha aliendelea kuongeza
kuwa viwango vya ubadilishaji fedha umeendelea kuimarika na upatikanaji wa
vyakula nao unakwenda vizuri.
Akiendelea kufafanua
Mhe. Dkt Mgimwa alisema katika “Mikutano hii ya majira ya kipupwe inayoendelea
hapa Washington inatupatia fursa ya kueleza hali tuliyofikia katika kuendesha
uchumi wetu, nafasi tuliyonayo kiuchumi, na tunapata nafasi ya kujieleza ni namna
gani Tanzania inavyoweza kukidhi mahitaji ya wananchi wake pamoja na utendaji wa
uchumi wetu. Aidha alisema kuwa Tanzania inapata nafasi ya kuishawishi dunia ili
iweze kutuunga mkono katika maeneo tunayowekeza.
“Katika mikutano
hii ya Majira ya kipupwe tunapata nafasi ya kuwa katika muda mzuri wa kupata
uwezekano wa kuyatatua matatizo yetu ya kiuchumi kwa kuwekeza zaidi ili vyanzo
vyetu tunavyowekeza viweze kutuletea maendeleo ya haraka”. Aidha Mgimwa
aliendelea kueleza kuwa hivi sasa Serikali inawekeza katika gesi iliyoko Mtwara
ili itumike kutoa umeme kwani bei yake ni ndogo ukilinganisha na bei ya mafuta
ambayo yanatumika. Aidha alisema kuwa Gesi hii itasaidia
viwanda kupata umeme na kuongeza ajira pamoja na mapato ya Taifa yatakuwa kwa
haraka zaidi.
“Serikali ina
mpango wa kupanua Reli, Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga na Bagamoyo ili
kurahisisha uingizaji wa mizigo na kukuza biashara kwa nchi zinazotuzunguka
pamoja na kurahisisha usafiri kwa wananchi kwa njia ya reli.” Aliongeza Mgimwa.
“Tumezungumzia
namna ya kuunganisha reli za nchi zinazotuzunguka kama vile Zambia, Burundi,
Rwanda na Uganda hivyo tunavyowaeleza hivi tunapata wawekezaji wengi
wanaotuunga mkono kwa kupitia Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Mpaka sasa hivi wameonyasha kwamba utendaji wa uchumi wa nchi yetu unakwenda
vizuri kwa hivyo wana imani kubwa na nchi yetu. Kwa kuwaeleza hivyo wao
wanaweka ushawishi kwa wawekezaji wakubwa walioko katika nchi zingine”. Alisema
Mhe.Dkt Mgimwa.
Mgimwa alimalizia
kwa kuwaomba wananchi kuwa, waunge mkono sera zinazowekwa mbele yao ambazo
zinaboresha uchumi, tunaomba wawekezaji binafsi katika sekta binafsi nao
watuunge mkono kwa kuwekeza katika miradi ambayo tunaiweka mbele yao ili
washirikiane kuiboresha na kuijenga Tanzania. Kila mtu atuunge mkono kwa sababu tunataka Tanzania ibadilike
na kuongeza kasi ya maendeleo ili kila mtu apate nafasi ya kuboreka kiuchumi.
Waziri
wa Fedha, Dk William Mgimwa akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Africa
Group (IMF) , Momodou Bamba Saho mara baada ya kumaliza majadiliano.
Ujumbe
kutoka Tanzania katika kikao cha pamoja na Mwakilishi Mkazi wa World
Bank Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Philippe Dongier katika
majadiliano kabla ya kukutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi wa Afica Group One Bw. Wilson Toninga Banda, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group One Bw. Denny H. Kalyalya pamoja na Mkurugenzi Mwandamizi wa Africa Group One Bw. Peter Larose wakiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dk. Willia Mgimwa.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi wa Afica Group One Wilson Toninga Banda, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group one Denny Kalyalya pamoja na Mkurugenzi Mwandamizi wa Africa Group One Peter Larose wakiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi wa Afica Group One Wilson Toninga Banda, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group one Denny Kalyalya pamoja na Mkurugenzi Mwandamizi wa Africa Group One Peter Larose wakiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dk. Willia Mgimwa.
No comments:
Post a Comment