Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, wakati wa kukagua Matanki ya kuhifadhia Maji eneo la Kimara Jijini, Dar es Salaam, hata hivyo matanki hayo yatabomolewa na kujengwa upya katika miradi ya Maji inayoendelea kujengwa.
Naibnu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoka katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kibamba, Dar es Salaam jana
SERIKALI KUMALIZA TATIZO LA MAJI
Serikali imesema itahakikisha miradi ya Maji
inayojengwa kutoka Ruvu na chini yote ina kamilika septemba mwakani
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla katika siku yake ya pili ya ziara ya kukagua miardi ya na Maji na
Vyanzo vyake vinavyomilikiwa na Shirika la Maji Taka na Safi Dar es Salaam (Dawasa)
Awali akiwa katika Shule ya Msingi Mavurunza iliyopo
kata ya Mavurunza katika Jimbo la Ubungo, nusura Mkutano wa hadhara uvunjike
kwa kile kilichoonekana ni ushabiki wa kisiasa kati ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa Chama Cha Demokrasi
na Maerndeleo (CHADEMA) waliokuwa wanabishana wakati viongozi wakizungumza
akiwemo Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika
Makalla aliendelea kwa kusema, Serikali imekwishatenga
pesa kwa ajili ya miradi hiyo ambayo miradi yote hiyo itagharimu sh milioni
Bilioni 397
Alisema
kama miradi hiyo itakamilika lazima tatizo la maji kwa wakazi wa Jimbo la
Ubungo na Dar es Salaam kwa ujumla litapungua kwa kiasi kikbwa sana kama siyo
kumalizika kabisa
Naye Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliwasihi wananchi kwamba miradi
hii inayotekelezwa ni ya wananchi wote wala haiangalii kichama wala kisiasa.
Naibu Waziri wa Maji kesho ataendelea na ziara
yake kwa siku ya tatu kwa kuendelea na kukagua miradi mablimbali ya Maji inayojengwa jijini
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment