MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, July 16, 2014

USHABIKI WA KISIASA WASABABISHA KUSITISHWA KWA MKUTANO WA NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA


Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Makongo baada ya kukagua utandazaji wa mabomba katika mradi mkubwa wa kupeleka maji katika matenki yaliyopo katika Chuo Cha Ardhi, Dar es Saam akiwa katika mfululizo wa ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya Maji


Baadhi ya wanachama wa CCM wakizuiana wasilete fujo wakati wa Mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla uliofanyika katika Kata ya Goba, Dar es Salaam hat hivyo Mkutno huo haukufanyika baada ya ubishani mkali na vugurugu kati ya wanachama wa Chadema na CCM


Dua Said aliyewahi kuichezea timu ya Simba akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa amejiunganishia Maji na kutengeneza Tenki analotumia kuhifadhia Maji ya Dawasco na kuyauza bila kuyalipia



Wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam wakichota Maji bure waliyokuwa wanauziwa kabla ya wamiliki kukamatwa wakiiba Maji


Askari wakilinda Nyumba zilizokutwa na tuhuma za kuiba Maji ya Dawsco eneo la Kigogo, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makalla akijianda kukagua Mradi wa Bomba kubwa la Maji linalojengwa eneo la Makongo Dar es Salaam

Hili ndilo Bomba la Maji  linalojengwa Makongo


Askari akilinda katika Mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla eneo la Goba

Wafuasi wa Chadema wakiwa na Mabango katika Mkutano wa Goba

Wafuasi wa CCM wakiwa na Mabango katika Mkutano uliofanyika Goba


Polisi wakiwa watuliza wafuasi wa Chadema na CCM


Polisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema katika Mkutano  uliofanyika Goba



No comments:

Post a Comment