Thursday, August 25, 2011
Wednesday, August 24, 2011
Mazishi ya Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Mussa Khamis Silima
Jeneza la Mwili wa Marehemu, Mussa Khamis Silima ukiingizwa kwenye kaburi wakati wa maziko yaliyofanyika katika kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja Zanzibar
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rai s, Dk Mohamed Gharib Bilali, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu Mussa Khamis Silima, aliyefariki Agosti 23 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22. Marehemu Silima amezikwa leo Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Tuesday, August 23, 2011
Mbunge wa Baraza la wawakilishi afariki Dunia
Mbunge wa Baraza la wawakilishi, Mussa Khamis Silima aliyepata ajali katika eneo la Nzuguni Dodoma akitokea jijini Dar es Salaam amefariki dunia katika Hospita ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha mifupa (MOI) alikokuwa anapatiwa matibabu akitokea katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Katika ajali hiyo alikuwa na Mkewe, Mwanakheri Twalib aliyefariki na kuzikwa jana mzjini Zanzibar, Dereva na Mtumishi wa ndani ambao wao walijeruhiwa na bado wanapatiwa matibabu. Taarifa za kifo zimetangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda Bungeni mjini Dodoma wakati wabunge wakichangia Hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2011/12. Bunge limeahirishwa hadi kesho
Monday, August 22, 2011
Ajali ya Mbunge wa Baraza la wawakilishi iliyotokea Dodoma
Hivi ndivyo gari ilivyoharibika baada ya kutokeav ajali ambapo mke wa Mbunge huyo, Mwanakheri Twalib alifariki
Mwili wa marehemu Mwanaheri Twalib ukitolewa katika Hospitali Kuu ya Dodoma tayari kusafirishwa kwa mazishi Zanzibar
Mwili wa marehemu Mwanaheri Twalib ukitolewa katika Hospitali Kuu ya Dodoma tayari kusafirishwa kwa mazishi Zanzibar
Friday, August 19, 2011
Makamu wa Rais katika Mkutano wa SADC, Angola
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikaguwa Gwaride lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga wakati alipokuwa akiondoka uwanja wa ndege wa Fevereiro uliopo jijini Luanda, Angola leo Agosti 19, baada ya kumalizika kwa mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana Agosti 18. Picha na Amour Nassor-OMR
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI ZA SADC NCHINI ANGOLA
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI ZA SADC NCHINI ANGOLA
AGOSTI 17-18, 2011
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika mkutano wake mkuu wa 31 ambao ulihusisha pia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa mwaka 2011/12, ambapo Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola amekabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba.
Akipokea nafasi hiyo, Rais Dos Santos alifafanua nia ya SADC kuendelea kushikamana na kudumisha amani katika nchi wanachama, huku akieleza kuwa suala la ukosefu wa ajira kwa wananchi wa nchi hizi hasa vijana linapaswa kutazamwa kwa jicho la karibu kwa kuwa ni sawa na bomu linaloweza kulipuka wakati wowote kama halitapatiwa ufumbuzi.
Katika mkutano huo mambo kadhaa yalijadiliwa na mengi yaliakisi hali ya amani na utulivu katika nchi wanachama na kubwa likawa kwa nchi hizi kukubaliana kwa kauli moja kutoa msaada wa hali na mali kwa nchi ya Somalia inayokabiliwa na baa la njaa. Nchi ya Afrika Kusini ilikubali kutoa usafiri wa michango yote itakayotakiwa kwenda Somalia wakati Tanzania ilitangaza kuhusu mchango wake ambao alikwishaahidiwa Rais wa Somalia Abdullah Yusuf Ahmed alipokuja kumtembelea Rais Jakaya Kikwete na kuomba msaada wa hali na mali kwa nchi yake, jambo ambalo lilikubaliwa kwa uharaka na Tanzania.
Mkutano huo licha ya kujadili suala la hali ya kisiasa nchini Zimbabwe na Madagascar, pia ulikamilika kwa kutiliana saini ya makubaliano katika mikataba mitatu baina ya nchi wanachama iliyohusu mashirikiano katika kudhibiti fedha chafu, Kupitishwa kwa katiba ya mashirikiano kwa majeshi ya Polisi katika nchi wanachama, sambamba na ule wa utunzaji wa mazingira katika ukanda wa Kavango na Zambezi.
Mkutano huo ulimchagua Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kuwa Mwenyekiti wa Kamati nyeti ya Siasa, Ulinzi na Usalama huku Makamu Mwenyekiti wake akichaguliwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania. Nafasi ya Mwenyekiti itabakia kwa mwenyeji wa mkutano huo Angola hadi mkutano mkuu mwingine utakapofanyika mwakani nchini Msumbiji na hivyo nchi hiyo kupewa jukumu hilo kwa mwaka 2012/13.
Katika mkutano huu nafasi ya Tanzania imebakia kuonekana kuwa ya kuigwa kutokana na kuwa na hali tulivu sambamba na kuwa eneo la kuigwa kulinganisha na mataifa mengine.
Katika mkutano huo; Makamu wa Rais aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Kilimo ambaye alitangulia Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Ulinzi ambaye pia alitangulia, Hussein Mwinyi na Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami.
Mlima Kilimanjaro waingizwa kwenye shindano la kutafuta maajabu saba ya Asili ya Dunia
Taasisi ya New7wonders ya Uswis inaendesha shindano la kutafuta maajabu ya asili ya Dunia. Taasisi hiyo imewahi kuandaa shindano kama hili mwaka 2007 ambapo ilishindanisha maajabu ambayo ni ya kutengenezwa na binadamu(made new7wonders). katika shindano hilo maajabu saba yaliyochaguliwa ni Chichenitza ya Mexico, christ Redeemer ya Brazil, Colosseum ya Italia, Taj Mahal ya India, Great Wall ya China, Machu Picchu ya Peru, Petra ya Jordan
Mwaka huu taasisi hiyo imeandaa Shindano hilo la kutafuta maajabu saba ya asilia ya dunia. Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa vivutio 28 duniani ambavyo vimefanikiwa kuingia katika hatua ya mwisho ya ushindani baada ya kushindanishwa na vivutio vingine kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kutoka bara la Afrika ni vivutio viwili tu vilivyoweza kuapata nafasi ya kuingia katika Kinyanga'nyiro hicho. Mlima Kilimanjaro wa Tanzania, na Table Mountain ya Afrika kusini
Mwisho wa kupiga kura ni mwezi novemba mwaka huu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige akizindua mtindo wa kupiga kura mjini Dodoma jana kupitia http://www.new7wonders.com/. Nyuma ya Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii, Aloyce Nzuki na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
Tuesday, August 16, 2011
Ziara ya warembo wa Miss Tanzania 2011 mkoani Arusha
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine wakicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli juzi mkoani Arusha. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa wamevalia vazi maalum livaliwalo na wanawake wa jamii ya Kimasaai wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo
Waipata cahakula
Sunday, August 14, 2011
Shirika la Nyumba la Taifa lazindua Ujenzi wa Nyumba za Makazi eneo la Medeli Dodoma
Ramani ya eneo la Medeli Dodoma ambapo patajengwa Nyumba za Makazi na Shirikan la Nyumba la Taifa (NHC)
Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaziwasanii wa kikundi cha tupendane wakitumbuiza
Mkurugezi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa uzinduziWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu muda mfupi baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Nyumba za Makazi
Saturday, August 13, 2011
Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini hatimaye yapitishwa na Bunge
Baadhi ya Wabunge wakimpongeza Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu Waziri wake , Adam Malima baada ya Bunge Kupitisha Bajeti ya Makadirio na Matumizi kwa mwaka 2011//12
Friday, August 12, 2011
Mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba na Balozi wa Marekani nchini, Alphonso Lenhardt
Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM) Peter Selukamba (kushoto) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini, Alphonso Lenhardt kwenye Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma kwa ajili ya kukutana kwa mazungumzo
Benki ya NMB yatoa msaada wa Sh Milion 10 kwa Taasisi ya WANA
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mark Wiessing ambaye Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam l. Fedha hizo zitatumia kwa ajili ya miradi ya uwezeshaji wa wanawake
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB (kushoto) na ShyRose Banji ambaye ni Afisa Mahusiano (kulia) katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10.
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimuonyesha kabrasha lenye kazi mbalimbali za WAMA Mark Wiessing ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB katika ofisi za WAMA Ikulu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10. Fedha hizo zitatumia kwa ajili ya miradi ya uwezeshaji wa wanawake
Wednesday, August 10, 2011
Luten Jenerali Mstaafu, Silas Mayunga aagwa Lugalo Dar es Salaam
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi, wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Viongozi wa Serikali, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agosti 10. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Msimu wa warembo wa Vodacom Miss Tanzania kuelekea Fainali
Baadhi ya warembo hao wanaowania Taji la Miss VodacomTanzania linalotarajia kufanyika Septemba jiji Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2011
Sakata la Uhaba wa Mafuta lachukua sura mpya Bungeni
Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba akitoa hoja ya dhalura Bungeni kuhusu sakata la mafuta linaloikabili nchi kwa takribani siku ya saba sasa Tnagu Mamla ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) kutangaza punguzo la bei ya Mafuta
Waziri wa Nisahti na Madini, William Ngeleja akitoa taarifa ya Serikali baada ya wabunge kujadili hoja ya Mbunge wa Bumbuli, January Makamba kuhusu tatizo la Mafuta lilijitokeza hivi karibuni
Subscribe to:
Comments (Atom)








