Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.) akipewa maelezo na Balozi wa China nchini, Bw. Liu Xinsheng (aliyeinama) kuhusu Baiskeli zilizotolewa kwake na Ubalozi huo. Ubalozi huo pia umemkabidhi Waziri mipira 300 kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu. Aidha, Ubalozi wa China umetoa vifaa vya michezo ya Kichina kwa Chama cha Wushu Tanzania. Vifaa hivyo vimetolewa leo katika Ubalozi wa China. (Picha na Concilia Niyibitanga- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)
Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam Serikali ya China imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwa ni pamoja na mipira 300 kwa Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano kati ya Serikali ya Tanzania na ya nchi hiyo. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Balozi wa China nchini Liu Kinsheng alisema licha ya kutoa mipira ya miguu, Serikali yake pia imetoa zaidi ya baiskeli 15 ambazo zitakwenda katika jimbo la Dr. Nchimbi pamoja na vifaa vya michezo ya kichina vitakavyokwenda katika chama cha michezo ya Kichina Tanzania (WUSHU). Akipokea msaada wa vifaa hivyo jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi alisema kuwa wengi wanahisi kuwa mpira wa miguu tu unapewa kipaumbele kwa misaada, tofauti na vyama vya michezo mingine kama vile ngumi na riadha ambazo pia vinahitaji msaada wa kifedha na vifaa. Dr. Nchimbi alisema wanamichizo ni sehemu ya Jumuia za Vijana ambao kama Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inawajibibu wa kusaidia kila inapowezekana ili kurudisha maendeleo ya michezo nchini. Nae Katibu Mkuu wa Chama cha Michezo ya Kichina Tanzania (WUSHU) Bwana Fred Maiga amesema vifaa hivyo ambavyo ni mapanga na vifaa mbalimbali vya mchezo huo vitasaidia kuendeleza mchezo wa kichina wa Simba na nyoka kwa vijana wa Kitanzania ambao mchezo huo umekuwa ukidorora siku hadi siku. “Tunaishukuru Serikali ya China kwa msaada wa vifaa vya mchezo wa nyoka na Simba kwani michezo hii imekuwa ikidorora siku hadi siku hivyo kwa msaada huu itaimarisha kwa kasi ukuaji wa michezo ya Kichina na hatimae tutakuwa na nafasi ya kuingiza timu katika mashindano ya OIympic. |
No comments:
Post a Comment