Mkuu wa Jeshi la Pilisi Tanzania (IGP) Said Mwema, akizungumza na waandishi wa habari leo Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam kuhusu matukio mbali mbali ya uhalifu sambamba na tishio la Ugaidi. IGP Mwema alisema kuwa Jeshi la Polisin limejipanga kikamilifu kudhibiti kila aina ya uhalifu na kuwataka wananchi wa kutoa taarifa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama pindi watakapobainiadalili za kutokea tukio lolote la kihalifu. IGP Mwema laiongeza kusema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga pia katika kukabiliana na Ugaidi wa Al Shaabab na aina nyingine za uharamia katika ukanda wa Afrika Mashariki. Picha na Victor Makinda
No comments:
Post a Comment