Ripoti ya Maendeleo ya Dunia 2011
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
“Uendelevu na Usawa: Mustakabali Bora kwa Wote”
Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2011 inatupatia tathmini na daraja
za Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2011 ya nchi 187 na ya
maeneo yanayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, sambamba na Farihisi ya
Tofauti ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2011, Farihisi ya Tofauti za
Kijinsia ya nchi 146, Farihisi ya Vigezo Mbalimbali vya Umaskini ya nchi
160.
Daraja za nchi na tathmini zinazoainishwa kwenye Farihisi ya Maendeleo
ya Dunia huwa hazitangazwi kabisa hadi uzinduzi unakapofanywa kwa
dunia nzima pamwe na kusambazwa kwa nakala ya kimtandao ya Farihisi ya
Maendeleo ya Dunia. Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2011
itatolewa mwezi Novemba.
Ni makosa kulinganisha tathmini na daraja hizi na zile za ripoti zilizopita,
kwa sababu vigezo vya takwimu na njia zinazotumika vimebadilika, pia
idadi ya nchi zilizojumuishwa kwenye Farihisi ya Maendeleo ya Dunia.
Nchi 187 zilizopangiwa daraja katika Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ya
Mwaka 2011 zinawakilisha ongezeko muhimu miongoni mwa nchi 169
zilizomo ndani ya Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2010, ambapo
viashirio vyenye kutoa habari muhimu za nchi nyingi havikuweza
kupatikana.
Wasomaji wanashauriwa kupima maendeleo kutumia viwango
vya Farihisi ya Maendeo ya Dunia kwa kuzingatia Jedwali Nambari 2
(Maelekeo ya Farihisi ya Maendeleo ya Dunia) kwenye Ambatanisho la
Takwimu la ripoti hiyo.
Jedwali Nambari Mbili lina msingi wake katika viashiria, mbinu na takwimu
za nyakati ambavyo ni thabiti, hivyo kuonyesha mabadiliko ya kweli
yaliyofikiwa kwenye kipindi kilichopita na kuonyesha maendeleo halisi
yaliyofikiwa na nchi hizo.
Kwa habari zaidi jinsi farihisi hiyo ilivyofikiwa tafadhali rejea kwenye
Hati ya Ufundi 1-4 katika Ripoti ya 2011 na nyaraka zilizopita zinazohusiana na maelezo hayo ambazo zinapatikana katika tovuti ya Ripoti
ya Maendeleo ya Dunia.
Farihisi ya Maendeleo ya Dunia
Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ni muhtasari wa kipimo cha kukadiria
maendeleo ya muda mrefu ya vigezo vitatu muhimu vya maendeleo ya
mwanadamu: Maisha marefu na yenye afya, uwezo wa kuufikia ujuzi, na
hali ya kuridhisha ya maisha. Kama ilivyo kwenye Farihisi ya Maendeleo ya
Dunia ya Mwaka 2010, maisha marefu na yenye afya hupimwa kwa
kuangalia wastani wa muda wa kuishi, urahisi wa kupata ujuzi hupimwa
kwa (i)wastani wa kiwango cha elimu ya watu wazima waliyopata watu wa zaidi ya umri wa miaka 25 na zaidi katika kipindi chao cha kuishi na (ii) miaka ya kusoma inayotarajiwa na watoto wenye umri wa kuanza darasa la kwanza iwapo desturi iliyopo ya wale wanaoorodheshwa kuanza masomo itabakia hivyo hivyo katika maisha yote ya mtoto.
Kiwango cha maisha kinapimwa na wastani wa kipato anachopata kila mtu
kwa mwaka kutoka kwenye Pato la Taifa la Mwaka. Ili kuhakikisha kwamba kuna ulinganishaji wa kutosha baina ya nchi na nchi, Farihisi ya Maendeleo ya Dunia huegemea zaidi takwimu za mataifa kutoka Kitengo cha Idadi ya Watu cha Umoja wa Mataifa, Taasisi ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia. Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi, tathmini na daraja za ripoti ya mwaka huu haziwezi kulinganishwa na ripoti za zamani (ikiwemo Farihisi ya Maendeleo ya
Dunia ya 2010) kwa sababu ya idadi ya masahihisho katika viashirio vilivyomo iliyofanywa na mashirika yenye mamlaka hayo. Ili kuwezesha upimaji leo wa maendeleo kufuatana na Viashirio vya Maendeleo ya Mwanadamu, Ripoti ya 2011 inajumuisha Viashirio vya Maendeleo ya Mwanadamu kuanzia mwaka 1980 hadi 2011.
Tathmini na daraja la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Kiwango cha tathmini ya Tanzania kwa mwaka 2011 ni 0.4866—
kinachoiweka kwenye kwenye kiwango cha chini cha maendeleo ya
mwanadamu—ambapo Tanzania ipo katika nafasi ya 152 kati ya
nchi na maeneo 187.
Kwenye Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya Mwaka 2010, Tanzania ilishika
nafasi ya 148 kati ya nchi 169. Hata hivyo, si sahihi kulinganisha tathmini na
daraja za sasa na zile za ripoti zilizo chapishwa zamani, kwa ni vigezo vya takwimu na namna ya kupima vimebadilika,vilevile idadi ya nchi zilizojumuishwa kwenye Farihisi ya Maendeleo ya Dunia.
Maendeleo ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania yalivyoainishwa na Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ni haya: Kati ya mwaka 1980 na 2011, wastani wa kuishi wa wakati wa kuzaliwa uliongezeka kwa miaka 7.7, ambapo wastani wa miaka ya kusoma shuleni uliongezeka kwa miaka 2.6 na kipindi kizima kilichotarajiwa kumaliza shule kiliongezeka kwa miaka 1.8.
Kipato cha kila mtu kwa mwaka kiliongezeka kwa asilimia 58.9 kati ya mwaka 1990 na 2011.
Table A: United Republic of Tanzania’s HDI trends based on consistent time series data, new component indicators and new methodology
| | Life expectancy at birth | Expected years of schooling | Means years of schooling | GNI per capita (2005 PPP$) | HDI value |
| 1980 | 50.5 | 7.3 | 2.5 | .. | .. |
| 1985 | 51.2 | 5.9 | 3.2 | .. | .. |
| 1990 | 50.6 | 5.5 | 3.6 | 0,834 | 0.352 |
| 1995 | 49.6 | 5.4 | 4.1 | 0,785 | 0.351 |
| 2000 | 50.4 | 5.4 | 4.6 | 0,839 | 0.364 |
| 2005 | 53.4 | 8.2 | 4.8 | 1,060 | 0.420 |
| 2010 | 57.4 | 9.1 | 5.1 | 1,272 | 0.461 |
| 2011 | 58.2 | 9.1 | 5.1 | 1,328 | 0.466 |
Figure 1 below shows the contribution of each component index to United Republic of Tanzania’s HDI since 1990.
Figure 1: Trends in United Republic of Tanzania’s HDI component indices 1990-2011

Kupima kiwango cha mandeleo kwa kulinganisha na nchi na nchi
Maendeleo ya muda mrefu ya nchi yanaweza kupimwa kwa kulinganishwa
na yale ya nchi nyingine---ikizingatiwa jiografia na kiwango cha nchi hiyo kama ilivyoainishwa na Farihisi ya Maendeleo ya Dunia. Mathalani, kwenye kipindi kati ya 1990 na 2011 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mauritania na Cote d’Ivoire zilionja viwango tofauti vya maendeleo vilivyoanza kuboresha nafasi zao katika Farihisi ya Maendeleo ya Dunia.
Farihisi ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya 2011 ya 0.466 iko juu ya
wastani wa 0.456 wa nchi zilizopo zilizopata maendeleo duni ya mwanadamu pia juu ya wastani wa 0.466 wa nchi za Kiafrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.
Miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazoikaribia Tanzania katika daraja ya Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ya 2011 na idadi ya watu ni Uganda na Cote d’Ivoire, ambazo zimewekwa kwenye daraja 161 na 170 kwa mpangilio wa kuzitaja.
Table B: United Republic of Tanzania’s HDI indicators for 2011 relative to selected countries and groups
| | HDI value | HDI rank | Life expectancy at birth | Expected years of schooling | Mean years of schooling | GNI per capita (PPP US$) |
| United Republic of Tanzania | 0.466 | 152 | 58.2 | 9.1 | 5.1 | 1,328 |
| Uganda | 0.446 | 161 | 54.1 | 10.8 | 4.7 | 1,124 |
| Côte d Ivoire | 0.400 | 170 | 55.4 | 6.3 | 3.3 | 1,387 |
| Sub-Saharan Africa | 0.463 | — | 54.4 | 9.2 | 4.5 | 1,966 |
| Low HDI | 0.456 | — | 58.7 | 8.3 | 4.2 | 1,585 |
No comments:
Post a Comment