TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 27, 2012
POLISI MORO YAACHA 17, TZ PRISONS 11
Klabu
tano za Ligi Kuu ya Tanzania zimewasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) majina ya wachezaji ambao zimewakatishia
mikataba/mikataba yao kumalizika au kuwaacha kwa ajili ya usajili wa
wachezaji msimu wa 2012/2013.
Kwa
mujibu wa klabu hizo, Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha
wachezaji 17 wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi
Msimu huu imeacha wachezaji 11. Azam imekatisha mikataba ya wachezaji
watatu.
Wachezaji
12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar wakati wakati
kwa upande wa Simba wachezaji waliomaliza mikataba ni wanne huku
ikionesha nia ya kuwatoa kwa mkopo wengine wanne.
Uhamisho
wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika
Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa
Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
Kwa
klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni
kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia
Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.
Wachezaji
walioachwa Polisi Morogoro ni Abdul Ibadi, Ally Moshi, Benedict
Kitangita, Hassan Kodo, Hussein Lutaweangu, Hussein Sheikh, Juma
Maboga, Mafwimbo Lutty, Makungu Slim, Mbaraka Masenga, Method Andrew,
Moses Mtitu, Ramadhan Kilumbanga, Ramadhan Toyoyo, Said Kawambwa, Salum
Juma na Thobias John.
Tanzania
Prisons imewaacha Adam Mtumwa, Dickson Oswald, Exavery Mapunda, Ismail
Selemani, Lwitiko Joseph, Mbega Daffa, Mwamba Mkumbwa, Musa Kidodo,
Rajab Ally, Richard Mwakalinga na Sweetbert Ajiro.
Wachezaji
waliomaliza mikataba yao kwa mujibu wa Kagera Sugar ni Cassian Ponera,
Hamis Msafiri, Hussein Swedi, Ibrahim Mamba, Martin Muganyizi, Mike
Katende, Moses Musome, Msafiri Davo, Said Ahmed, Said Dilunga, Steven
Mazanda na Yona Ndabila.
Azam
imewasitishia mikataba wachezaji Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino
Augustino. Wachezaji waliomaliza mikataba Simba kwa mujibu wa klabu
hiyo ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago, Juma Jabu wakati
Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu.
Wachezaji ambao Simba inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina.
DODOMA YAITAMBIA MBEYA COPA COCA-COLA 2012
Dodoma
imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012
baada ya leo asubuhi (Juni 27 mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao 2-0
katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha mkoani Pwani.
Mabao
ya Dodoma katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu
dakika ya 59 wakati Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi dakika
saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupachika bao la pili.
Nayo
Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi ya kundi B
iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Mechi
za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati ya Arusha na Kusini Pemba
kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora kwenye Uwanja wa
Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na kutokuwepo
mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro Road) kutoka mkoani Pwani
kuingia Dar es Salaam.
Leo
jioni kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Ruvuma (Tanganyika Packers),
Mwanza na Tanga (Nyumbu), Kaskazini Unguja na Mara (Tamco) na Singida
na Kagera (Karume).
No comments:
Post a Comment