Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua
waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini
Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.
Waamuzi
hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya
vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12
na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa
CECAFA.
Kwa
upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony
Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara),
Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali
(Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Waamuzi
wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia
(Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara),
Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud
(Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment