Thursday, July 5, 2012
Makamu wa pili wa Rais akabidhi Vifaa vya Zahanati
Baadhi ya wageni waalikwa
wakiwa kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya huduma na tiba
kwa Zahanati ya Kimara. Kulia (Mwenye koti) ni Diwani wa Kata hiyo ya
Kimara kwa tiketi ya Chadema.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi vifaa vya
huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dk.
Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye
Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh. milioni 5.1,
vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya
Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia
ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni,
Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga
Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk. (Picha na
Bashir Nkoromo)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment