Tuesday, July 3, 2012
Bungeni Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla akijibu swali la Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika, alilouliza kuhusu Baadhi ya Viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi na kushindwa kutunzwa na mmiliki
Akijibu swali hilo Naibu Waziri alisema Chama cha Mapinduzi hakijashindwa kutunza viwanja hivyo maana mpaka sasa vinatumika katika Michezo mbalimabili na kuhusu viwanja hivyo kujengwa na wanachi wote wa Tanzania na kwanini vimilikiwe na Chama cha Mapinduzi, Makala alisema Viwanja hivyo vilijengwa na CCM wakati wa Chama kimoja kwa hiyo kama kuna watu wanataka wawe sehemu ya umiliki wa Viwanja hivyo wahamie katika Chama cha Mapinduzi
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma
Katika hatua nyingine baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika ndipo hoja ya mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Menejimenti yaUtumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Utawala Bora na Mahusiano na uratibu iliendelea kujadiliwa na wabunge mablimbali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment