![]() |
Cables: "MUHIMBILI"
Postal Address:
Telephones: 255-22-2151367-9 P.O. BOX 65000
Fax: 255-22-2150234 DAR ES SALAAM
Huduma katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea
kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.
Tathimini iliyofanyika kuanzia
asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara
ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika
kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha
Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama
kawaida.
Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine
wawili wako likizo na Registrar watatu
kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo
Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja
kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.
Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko
masomoni.
Upande wa Emergency Medicine,
Registrars wote 10 walikuja kazini.
Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini
wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo,
upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa
kufanyiwa upasuaji..
KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 1, 2012
No comments:
Post a Comment