Meneja Uhusinao wa Airtel,
Jackson Mbando, akizungumza katika uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao
ijulikanayo kama “kula Dabo” kupitia huduma ya Airtel Money. Uzinduzi wa
promotion hiyo ameufanya leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya
Kimataifa Dar es Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara
ya Kilwa jijini.
Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando,(aliye chuchuma mbele) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya vijana wanaotoa huduma mbalimbali katika banda la Airtel, baada ya uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo” kupitia huduma ya Airtel Money. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini
Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando, akizungumza katika uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo” pia alimpigia simu mteja mmoja mara baada ya kuibuka mshindi wa zawadi za papo kwa papo ndani ya saba saba. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini. Kulia ni Ofisa wa Airtel Money, Bahati Straton
Afisa wa Airtel 3G, Teher Abdulrahman, akichagua kikaratasi cha mshindi katika Bahati nasibu ya Papo kwa Papo katika viwanja vya sabasaba ndani ya Kijiji cha Airtel. Kushoto ni Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando na Katikati ni Ofisa wa Airtel Money, Bahati Straton, Airtel pia ilizindua promotion ya “Kula Dabo” kwa wateja wao watakao nunua bidhaa kwa Airtel Money
KAMPUNI
ya simu za mkono ya Airtel Tanzania jana imezindua promosheni kwa wateja
inayojulikana kama “Kula Dabo” katika maonyesho ya 36 ya biashara kwenye
viwanja vya Sabasaba Temeke.
Akizindua
promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando alisema
kuwa katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inamfikia kila Mtanzania na
kupunguza changamoto mbalimbali za kifedha.
Alisema
kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imeamua kuwazawadia wateja wake wote
wanaonunua salio kupitia simu za mknoni kupata mara mbili ya salio lolote
atakaloongeza kupitia Airtel Money na ataweza kupiga simu na kutuma sms
kwenda mtandao wowote
Promosheni
hii itaendelea katika msimu huu wa sabaSaba ambapo itadumu kwa muda wa wiki
mbili kuanzia sasa
Mmbando
alisema “ Airtel kwa kuonyesha tunawajali wakala wetu wote, mwezi huu kila
wakala atapata mara mbili ya kamisheni yake, lengo letu ni kuhakikisha kila
mdau wetu anafaidika na huduma yetu hii ya Airtel money”
“Wakala
wetu sasa mnakila sababu ya kuhakikisha mwezi huu unafanya mhamala mingi ili tu
muweze kupata kamisheni nyingi kwa kula dabo yako” aliendelea kusema Mmbando
Vilevile
mbali na kuwepo kwa promosheni ya kula dabo wateja wa Airtel watakaonunua
bidhaa mbali mbali katika viwanja na banda lete la sabasaba kupitia huduma yetu
ya Airtel money wataweza kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo pesa taslim
kuanzia shilingi 2,000, simu za mkononi aina ya Samsung 1085 pamoja na modem ya
3.75G kupitia droo ya kuchanganya kuponi itakayofanyika katika viwanja hivyo
kila siku saa nane kamili.
Airtel
tunawakaribisha wateja wetu kutembea kijiji cha Airtel katika Maonyesho ya 36
ya biashara ambayo yataendelea kwa muda wa siku kumi ili kujipatia huduma zetu
mbali mbali ikiwemo ya Airtel Money, kuwezesha simu yako kutumia intaneti yenye
spidi, kujipatia modem za 3.75G kwa gharama nafuu zaidi pamoja na kujua huduma
nyingine nyingi kutoka Airtel
Airtel
hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na
mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa ajira kwa
watanzania wengi kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza
kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, kwa wateja wetu wote Airtel money ina
mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima na kupitia huduma ya
Airtel Money unaweza kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote nchini na
utaweza kutuma kuanzia shilingi 1,000 hadi kiwango cha shilingi 1,000,000 kwa
Airtel money.
Maonyesho
ya kimataifa ya Dar es salaam Maarufu kama sabasaba, Ni maonesho ya kibiashara
yanayoongoza Tanzania maonyesho hayo yanayofanyika kwa siku kumi huvutia wageni
zaidi ya milioni nne na kujenga mahusiano na maingiliano baina ya watoa huduma
na wateja wao na kutoa fursa kwa wateja kuangalia na kulinganisha ubora wa
bidhaa.
No comments:
Post a Comment