HOSPITALI YA TAIFA
MUHIMBILI
|
Cables:
"MUHIMBILI" Postal Address:
Telephones: 255-22-2151367-9 P.O. Box 65000
FAX: 255-22-2150534
DAR
ES SALAAM
HUDUMA
ZAENDELEA KUIMARIKA MUHIMBILI
Leo huduma za tiba katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili zimeendelea kuimarika katika maeneo mengi. Taarifa kutoka
Kurugenzi ya Tiba (idara ya tiba, idara ya magonjwa ya dharura, idara ya
wagonjwa wa nje, idara ya magonjwa ya afya ya akili, na idara ya watoto) na
Kurugenzi ya Upasuaji (idara ya upasuaji, idara ya magonjwa ya wanawake, idara
ya meno, idara ya magojwa ya masikio, pua na koo, idara ya macho, na idara ya
nusu kaputi) imeonyesha kuimarika kwa huduma kwa kiwango kikubwa ukilinganisha
na hali ilivyokuwa siku chache zilizopita. Ifuatayo ni thathimini iliyofanyika
kuanzia asubuhi saa 2:00 hadi saa 11 jioni leo tarehe 4 Julaiy, 2012.
Kurugenzi ya Tiba
Idara ya Tiba: (Internal Medicine)
Madaktari walioko katika mafunzo kwa
vitendo (Interns) 11wamefika kazini na kufanya kazi. Registrar’s wote
wamefanya kazi, Madaktari Bingwa wote wamefanya kazi. Service ward rounds
zimefanyika pamoja na kliniki ya HIV imefanyika.
Idara ya Magonjwa ya Dharura:
(Emergency Medicine)
Madaktari waliokuwepo ni Daktari
Bingwa mmoja, Registrars wawili na pamoja na Interns wawili.
Idara ya Wagonjwa ya Nje (Cold OPD)
Registrars wote walikuja kazini na
wawili wana ruhusa maalum. Wagonjwa wote waliofika walionwa.
Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili
(Psychiatry and Mental Health)
Madaktari Bingwa wote walikuwepo
kazini isipokuwa mmoja ambaye yuko masomoni. Kliniki zote zimefanyika, wagonjwa
wote waliolazwa wodini wameonwa
Idara ya Watoto: (Pediatrics and Child
Health)
Madaktari Bingwa wote wamekuja kazni
na kufanya kazi. Interns watatu nao walikuja na kufanya kazi.
Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU)
Huduma kwa wagonjwa wote waliolazwa
chumba cha wagojwa mahututi wameonwa na wanaendelea kuhudumiwa chini ya
uangalizi wa karibu..
Kurugenzi ya Upasuaji
Upasuaji leo umefanyika na kuna
ongezeko kubwa la madaktari lililojitokeza leo kwa ajili ya kufanya upasuaji
katika vyumba vya upasuaji. Orodha ya wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji kesho
Alhamisi Julai 4, 2012 imeandaliwa na wagonjwa wote wamefanyiwa taratibu zote
kwa ajili ya upasuaji ikiwemo kushauriwa na kukubali kufanyiwa upasuaji, kupimwa
viwango au wingi wa damu kama inatosha mgonjwa kufanyiwa upasuaji pamoja na
taratibu nyingine za tiba. Hata hivyo, wagonjwa bado ni wachache wanaokuja
kliniki na waliolazwa wodini.
Idara ya Upasuaji: (General Surgery)
Idara ya Upasuaji wagonjwa walionwa na
Madaktari bingwa tu, hapakuwa na Interns wala Residents. Kliniki zote
zilizopangwa kufanyika leo zimefanyika hususani kliniki ya masikio, pua na koo
(ENT), magonjwa ya wanawake, macho (ophthalmology), matumbo (gastroentology),
njia ya haja ndogo kwa wanaume (urology), ngozi (skin), ART, magonjwa ya moyo
(cardiovascular), meno, plastic surgery pamoja na pediatric surgery. Aidha
kliniki zote kwa ajili ya wafanyakazi na wagonjwa wa kulipia (private) zote
zimefanyika
Idara ya Magonjwa ya Wanawake: (Obstetrics
and Gynaecology)
Wagonjwa wote waliolazwa wameonwa na
Madaktari Bingwa kwa kushirikiana na Interns wachache waliokuwepo.
Idara ya Meno: (Dental Surgery)
Madaktari waliokuwa zamu walipita
round na waliona wagonjwa wote waliolazwa.
Idara ya Masikio, Pua na Koo:
(Otorhinolaryngology)
Makaktari Bingwa walipita wodini kuona
wagonjwa waliolazwa na kufanya upasuaji kwa wagonjwa wawili.
Idara ya Nusu Kaputi: (Anaesthesia)
Madaktari Bingwa na wasaidizi wao
walikuwepo na kuendelea na kazi kama kawaida.
Idara ya Macho: (Ophthalmology)
Madaktari Bingwa waliona wagonjwa wote
waliolazwa wodini, waliendelea, kliniki na kufanya upasuaji.
Vyumba vya upasuaji: (Theatre)
- Urology: Walikuwa na orodha ya upasuaji na walifanya upasuaji wa mtu mmoja.
- Pediatric Surgery: Hawakuwa na orodha ya upasuaji kwa siku ya leo
- Plastic Surgery: Hawakuwa na orodha ya upasuaji.
- Otorhinolaryngology (ENT) Walikuwa na orodha, walifanya upasuaji kwa wagonjwa wawili.
- Macho: Wamefanya zote zilizotakiwa
Kurugenzi ya Tiba Shirikishi
(Clinical Support Services)
Madaktari wa Radiolojia wote nane
walikuwepo kazini na wamefnya kazi. Hata hivyo eneo hili halikuwa katika mgomo.
Upande wa Maabara: huduma zote ziliendelea kutolewa. Pia eneo hili halikuwa
katika mgomo.
Idara ya Pharmacy yenye iliendelea
kufanya kazi na pia haikuwa katika mgomo. Idara hii pia ina Interns
30 na kati yao watatu wako likizo mmoja yuko likizo ya uzazi waliobaki 27 wote
walikuwa kazini na kuchapa kazi.
Idara hii ina Wafamasia 12 ambapo 10
kati yao walikuwepo, na wawili wana likizo maalumu. Pharmacy zote zimefunguliwa
na kufanya kazi. Eneo hili pia halikuwa kwenye mgomo.
Kurugenzi ya Uuguzi na Ubora
(Nursing Services and Quality)
Wauguzi wote wanaotakiwa kuwepo kazini
wapo na wanaendelea na kazi. ha
Tathimini ya jumla:
Huduma zimeendelea kuimarika. Wagonjwa
ni wachache. Madaktari wengi wamerudi kazini na wanachapa kazi.
.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 4, 2012
No comments:
Post a Comment