MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, July 6, 2012

Kampuni ya Airtel yakabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kila siku ya Airtel Money


Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabithi bwn Bernard Chezue modem baada ya kuibuka kuwa mshindi wa droo ya kila siku inayowawezesha wateja wa Airtel waliofanya malipo ya bidhaa
katika viwanja vya sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa
Mshindi wa droo ya kila siku ya Airtel money bwana  Frank Joakim Mgumba akijaribu kutumia simu yake mara baada ya  kuibuka kuwa mshindi katika droo  inayohusisha wateja wa Airtel walionunua bidhaa kwa
kupitia Airtel money katika maonyesho ya Sabasaba.  Pichani Katikati ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde pamoja na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja wa viwanja vya sabasaba.

Mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa akichezesha
droo ya kuchagua mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kila siku iliyofanyika jana katika viwanja vya sabasaba ambapo wateja watano walionunua bidhaa kwa kupitia huduma ya Airtel money walijishindia
zawadi mbalimbali ikiwemo simu, modem na muda wa maongezi. Wakishuhudia pichani ni wafanyakazi wa Airtel


Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mshindi wa droo ya kila siku Bw Rucha Selemani modem baada ya kuibuka kuwa moja kati ya washindi  wa siku , droo hiyo inahusisha wateja waliofanya malipo ya bidhaa kupitia Airtel money katika viwanja  vya Sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Heleni Kimati




Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliko jiji Dar es salaam wakipata maelekezo  kuhusu huduma ya internet ya 3.75G kutoka kwa mfanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja  baada ya kutembelea banda la Airtel lililopo katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba 6 

No comments:

Post a Comment