|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali MohamedShein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd,Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, wakijumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika dua maalum ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya Meli ya Mv Skagit, iliyotokea hivi karibuni karibu na Kisiwa na Chumbe Zanzibar. Dua hiyo maalum imefanyika leo Julai 22 katika Msikiti wa Mwembe Shauri mjini Zanzibar.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, baada ya dua maalum ya
kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya Meli ya Mv Skagit, iliyotokea hivi karibuni karibu na Kisiwa na Chumbe Zanzibar. Dua hiyo maalum imefanyika leo Julai 22 katika Msikiti wa Mwembe Shauri mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment