Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wakipata maelezo ya maendeleo ya
uchimbaji wa gesi asilia nchini Tanzania walipotembelea makao makuu ya
British Gas (BG Group), ambayo imewekeza kiasi cha Pauni 80 za
Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia
nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema
gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mkoa wa
Pwani na Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG
Group mjini Reading, Uingereza, ambako Rais Kikwete na ujumbe wake
walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia
unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21
katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
|
No comments:
Post a Comment