THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliondoka
nchini usiku wa kuamkia leo, Jumanne, Julai 10, 2012 kwenda London, Uingereza kushiriki mkutano wa
kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani.
Rais
Kikwete ni miongoni mwa wakuu wa nchi tatu kutoka Afrika walioalikwa kushiriki
katika mkutano huo wa siku moja ulioitishwa na kudhaminiwa na Serikali ya
Uingereza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Taasisi ya
Bill and Belinda Gates Foundation.
Mbali
na Rais kikwete, viongozi wengine wa Afrika walioalikwa kwenye mkutano huo
ambao pia utahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun
ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Mkutano
huo utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Queen Elizabeth ni wa kwanza wa
aina yake duniani na utaanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha
wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari,
huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo
mwaka 2020.
Aidha,
mkutano huo ni nafasi ya pamoja ya kuiwezesha jumuia ya kimataifa kuonyesha
dhamira zaidi katika huduma za uzazi bora ambazo kwa kiasi fulani zitachangia
kuongeza kasi katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia nambari nne
(kupunguza vifo vya watoto) na nambari tano (kuboresha afya za akinamama).
Vile
vile mkutano huo ni nafasi ya jumuia ya kimataifa kuonyesha dhamira zaidi
katika kuboresha sera za uzazi bora na kupata michango zaidi ya raslimali
kutoka kwa nchi zinazoendelea, wafadhili, sekta binafsi na jumuia za kiraia kwa
nia ya kuboresha shughuli hizo.
Inakadiriwa
kuwa zitahitaji kiasi cha dola za Marekani bilioni 10 kwa miaka minane ijayo
kuanzia sasa 2012 hadi 2020 ili kudumisha huduma za sasa za uzazi bora duniani.
Kiasi cha dola bilioni nne za ziada
zitahitaji ili kuweza kuwafikisha wanawake milioni 120 katika nchi masikini
zaidi ambao kwa sasa hawapati huduma hizo katika miaka hiyo minane ijayo.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
10 Julai, 2012
No comments:
Post a Comment