JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Bw. Asah Andrew Mwambene ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia
tarehe 01 Julai, 2012. Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi
na Bw. Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko
Zanzibar.
Idara ya Habari
(MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa
Serikali hapa nchini.
IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI
NA MICHEZO
AGOSTI 1, 2012
No comments:
Post a Comment