MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Tuesday, September 4, 2012

Umoja yachezesha bahati nasibu ya kwanza

 Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Hemed Abdallah (kushoto) akiangalia wakati wa kuchezesha Bahati nasibu ya kwanza ya umoja iliyofanyika Dar es Salaam, wengine katika Picha, Meneja Maendeleo baishara, Linas Kahisha, Ofisa msaidizi wa Utawala, Getrude Biduka

    Umoja Switch ni Mtandao unaomilikiwa na mabenki kwa ajili ya kutoa huduma za kifedha. kwa sasa mtandao unatoa huduma za Umoja ATM zinazopatikana katika benki 24 ndani ya Tanzania bara na visiwani kwa gharama nafuu
Lengo kubwa ni kumsaidia mwananchi wa kiatnzania kwa kumrahisishia kupata fedha yake au kufanya malipo mengine kwa urahisi, ikiwa mahali popote na pia kwa gharama nafuu zaidi kuliko mitandao mingine

Mteja yeyote anaweza kupata huduma zote zitolewazo na ATM ya benki yoyote iliyo na nembo ya Umoja. kinachotakiwa ni kwenda kwenye benki yeyote iliyo ndani ya mtandao wa Umoja na fungua akaunti na unaweza kuchukua Kadi ya ATM
   Katika promoeshini iliyozinduliwa jana mteja atakayetumia sana kadi ya ATM ya Umoja atajinyakulia Sh laki moja kila mwisho wa mwezi na Sh Laki mbili zitatolewa kwa wateja waliotumia mpya za ATM za Umoja
 
No comments:

Post a Comment