Mkuu wa Kitengo cha Taarifa rasmi katika Sekretarieti ya Tume ya mabadiliko ya Katiba, Hanifa Masaninga akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza la wawakilishi Zanzibar majukumu ya Kitengo hicho wakati walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Tume tarehe 17 Septemba, 2012. Wa tatu kulia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ali Abdalla Ali na wa pili kulia ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti katika Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mohamed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo hicho kwa Wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wakati walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Tume hiyo, leo jumatatu tarehe 17 Septemba, 2012. Wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Ali Abdalla Ali na mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Musa Ali Hassan.
No comments:
Post a Comment