MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, October 25, 2012

Hafla ya Kuhitimisha Maadhimisho ya Miaka Hamsini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika wakati wa hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya miaka Hamsini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika jana.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (katikati), Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Fulugens Kazaula (kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mkandara, wakiwa katika maadhimisho ya miaka Hamsini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika jana.



VURUGU ZA ZANZIBAR VIONGOZI WA UHAMSHO WAFIKISHWA MAHAKAMANI
 Mmoja ya Kiongozi wa Jumuia ya Uamsho na Mihadhara ya Dini ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) , Shekh Suleiman Juma akitoka katika Mahakama kuu Vuga kujibu mashataka yanayomkabili yeye na wenzake.
 
VIONGOZI wa Jumuia ya Uamsho na Mihadhara ya dini ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakiingia katika gari ya Polisi wakiwa nje ya Mahakama kuu ya Zanzibar walipofikishwa kujibu makosa yanayowakabili likiwemo la kushawishi watu kufanya fujo za makusudi na kusababisha kuvuruga amani ya Nchi, kulia ni Shekh Farid Hadi na Sheikh Azzan Khalid.(Picha na Haroub Hussein).
 

No comments:

Post a Comment