Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya
mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ili kupitisha mechi
ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) kati ya Taifa Stars na Kenya (Harambe Stars) itakayochezwa
Novemba 14 mwaka huu jijini Mwanza.
Mechi
tano za ligi hiyo zilizokuwa zichezwe Novemba 11 mwaka huu,
zimerejeshwa nyuma kwa siku moja ambapo sasa zitafanyika Novemba 10
mwaka huu. Mechi hizo ni Simba vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa),
Kagera Sugar vs Polisi Morogoro (Uwanja wa Kaitaba) na Oljoro JKT vs
Ruvu Shooting (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Nyingine
ni Tanzania Prisons vs JKT Ruvu (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine) na
African Lyon vs Mtibwa Sugar (Azam Complex). Mechi ya Mgambo Shooting
vs Azam (Azam Complex) yenyewe itachezwa Novemba 10 mwaka huu kama
ilivyokuwa imepangwa.
Nayo
mechi ya Coastal Union vs Yanga (Uwanja wa Mkwakwani) itabaki Novemba
11 mwaka huu kwa vile Novemba 10 mwaka huu uwanja huo utakuwa na mechi
nyingine. TFF imepanga utaratibu wa kuwapata kwa wakati wachezaji wa
Yanga walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Mabadiliko
mengine ni ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mechi ya Villa Squad
vs Transit Camp iliyokuwa ichezwe Novemba 8 mwaka huu sasa inachezwa
Novemba 9 mwaka huu, na ile ya Novemba 7 mwaka huu kati ya Burkina Faso
na Small Kids inachezwa Novemba 9 mwaka huu. Viwanja ni vilevile.
Kamati
ya Ligi imelazimika kufanya mabadiliko hayo kutokana na viwanja husika
kuwa na mechi nyingine, na vilevile Small Kids kupata matatizo ya
usafiri kutoka mkoani Rukwa kwenda Morogoro.
No comments:
Post a Comment