Mkutano wa Tisa wa Bunge kuahirishwa leo, Kabla ya kusomwa kwa hotuba ya kuahirisha Bunge na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Bunge litaanza kwa kipindi cha maswali na majibu na kufuatia na mjadala wa hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyoiwasilisha Bungeni jana kuhusu Serikali kuchukua hatua dhidi ya watanzania walioficha fedha haramu nje ya nchi. pamoja na hoja hiyo pia Bunge litapokea hoja binafi za wabunge wengine ikiwa ni pamoja ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Mchemba inayohusu, Mswada wa Sheria ya uanzishwaji wa Mufuko wa Elimu ya Juuu, Hoja binafsi ya Mbunge wa Kuteuliwa , James Mbatia kuhusu udhaifu ulioko katika sekta ya Elimu nchini, Hoha binafi ya Mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangalla kuhusu Serikali ianzishe mpango maalum wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha Mfuko wa mikopo ya vyama wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo, Hoja ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuhusu mwenendo wa Baraza la Mitihani la Taifa unavyoathiri Elimu nchni, pamoja na hoja ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuhusu hatua za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughurikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment