MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, November 8, 2012

Uzinduzi wa Huduma ya Afya kwa Jamii


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mkurugenzi  Mkuu wa Hospitali ya Muhimbili  Dkt. Marina Njelekela wakati wa Uzinduzi wa Huduma  ya Afya kwa Jamii Viwanja vya Mnazi Mmoja  mjini Dar es Salaam  leo ,mgeni rasmi akiwa Mama Kikwete
Mwenyekiti wa Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mke wa Rais Mama Salma  Kikwete  akitoa Risala  wakati wa Uzinduzi wa Huduma ya Afya kwa Jamii  Viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Dar es Salaam leo  akiwa Mgeni rasmi.
Baadhi ya Akina mama waliofika Viwanja vya Mnazi Mmoja kupata Elimu mbalimbali kwa ajili ya Afya wakimsikiliza Mwenyekiti wa Wanawake na Maendeleo  (WAMA) Mama Salma Kikwete akizindua Huduma ya Afya  kwa Jamii  akiwa mgeni rasmi  jijini Dar es Salaam
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Wanawake na Maendeleo  (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwaeleza akina mama kuwahi Clinik wanapopata Ujauzito sio kusubiri mpaka mimba zikiwa kubwa ni hatari sana alisisitiza , wa  pili kulia  ni Mwenyekiti wa chama cha Madaktari Wanawake (MEWATA) akisikiliza kwa makini wakati wa Uzinduzi wa Huduma ya Afya kwa jamii akiwa mgeni  rasmi kwenye  hafla hiyo Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 

No comments:

Post a Comment