CHAMA cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimemfungia mchezaji Sued Lucas wa Boom FC kwa
mwaka mmoja baada ya kupatiakana na hatia ya kusaini timu zaidi ya moja.
Mchezaji huyo licha ya
kufungiwa, klabu yake ya Boom FC, imetozwa faini ya Sh 200,000.
Kamati ya Rufaa ya DRFA,
iliyokutana Aprili 11 mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Salehe Njaa,
kupitia Kanuni ya 50 (a) imemfungia
mchezaji huyo Sued Lucas kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuitoza klabu yake
faini ya Sh 200, 000 kwa mechi zote alizocheza na matokeo ya mechi zote
alizocheza mchezaji huyo yatabaki kama yalivyo.
Mchezaji huyo alisaini Boom
FC kwa kutumia jina la Sued Lucas, wakati huo huo akasaini timu ya Kumbukumbu
kwa jina la Issa Rashid Mwamlima.
Hivyo Kamati ya Rufaa
imeirudishia Boom FC pointi zake tatu na mabao 2-0, waliyoupata katika mechi
yao dhidi ya Kumbukumbu, iliyochezwa Aprili Mosi mwaka huu, uwanja wa Msasani.
Hatua hiyo ilifikiwa baada
ya Kumbukumbu kumwekea pingamizi mchezaji huyo dhidi ya Boom.
DRFA inapenda kusisisitiza uadilifu
kwa wachezaji na kuheshimu Kanuni na taratibu zilizowekwa, kwa maslahi na
maendeleo ya mpira wa miguu.
Kutokana na hatua hiyo, Ligi
Daraja la Pili, iliyokuwa ianze Aprili 9, ilisitishwa na sasa itaanza kesho
Aprili 15 kwa mechi tatu.
Boom FC watacheza dhidi ya Shariff
Star uwanja wa Airwing, Abajalo dhidi ya Red Coast, uwanja wa Shule ya Msingi
Mwalimu Nyerere na Friends Rangers watachuana na Day Break, uwanja wa Kinesi.
Imetolewa na Ofisa Habari wa
DRFA
Mohamed Mharizo
No comments:
Post a Comment