MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Wednesday, April 10, 2013

LOWASA ATOA MSAADA WA SH MILIONI TANO KWA BARAZA LA MSKITI TANZANIA

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA), Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung'he waliofika ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa Sh Milion. 5 kwa ajili ya kuendeleza mpango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Edward Lowassa akikabidhi msaada wa Sh mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA), Alhaj Juma Swalehe
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada wa Sh. Mil 5 kwa Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzana
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akizungumza baada ya kupokea msaada huo wa Sh Milioni tano kutoka kwa waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa

No comments:

Post a Comment