Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipozungumzia swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.
Rais
wa mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan
Mwinyi amevitaka vyombo vya habari nchini kusaidia wananchi kwa kutoa habari
njema na kuepukana na habari za uchochezi zinazoweza kuitenganisha jamii na
kuvuruga amani iliyopo nchini.
Mzee
Mwinyi ameyasema hayo leo, Jumatano, April
17, 2013 nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam katika mkutano na
waandishi wa habari aliouitisha kufafanua kauli aliyoita hivi karibuni kuhusu
kuchinja, na kuripotiwa kwa namna ambayo imeleta maana nyingine na kusababisha
malumbano.
Rais
huyo Mstaafu alisema kwamba Tanzania haina dini bali watu wake ambao ni wamoja
ndiyo wenye dini, na kusisitiza kwamba si vyema wananchi wakabaguana kwa imani
za kidini jambo ambalo amelitaja ni la hatari kwa mustakabali wa amani katika
Taifa.
Kuhusu
kauli aliyotoa, Mhe. Mwinyi alisema: "Si kweli Mzee Ruksa katoa ruksa ya
watu kutengana, Sikutoa ruksa hiyo. Hivyo, kama watu wana dharura (katika suala
la kuchinja) wavumiliane kama ilivyokuwa toka enzi za ukoloni wa Ujerumani na Uingereza”.
"Nilichokisema
ni kwamba kama mtu anachinja kwa matumizi yake na kundi lake asiingiliwe, ila
kama ni kwa biashara hapo ni lazima kuwa waangalifu kwa kuzingatia maamrisho ya
dini zetu”.
"Ni
vyema tukubaliane kwamba kwa miaka mingi toka utawala wa Ujerumani, Uingereza
na hivi leo miaka 50 baada ya Uhuru hakukupata kuwa na changamoto kama hii -
Kuna nini sasa hadi tukosane?”
"Mimi
nitakuwa mtu wa mwisho kuona Waislamu na Wakristo wakitengana maana utakuwa
mwanzo na mwisho wa wetu maana tutatengana kwa kila jambo. Huu ni wakati wa
kusogeleana", aliongezea.
Alihimiza
kuwepo kwa mazungumzo ya pande zote mbili ili kuendeleza muelewano wa enzi na
enzi, na pia aliwaomba wazee wenzie wasaidie katika kuzungumzia kutatua suala
hili. "Wazee lazima tulisemee suala hili na nyie wanahabari msaidie
kueneza habari njema ambazo zitasaidia kutuliza wananchi"
Aliwataja
wanaochochea suala la kuchinja kuwa ni watu watundu ambao wanatakiwa
kuelimishwa kwamba wanachokifanya si jambo jema na linahatarisha amani na
utulivu wa taifa letu
"Mtengano
huo hautoishia hapo kwenye kuchinja. Na kwa nini tutengane?"
alisema.
No comments:
Post a Comment