MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, April 21, 2013

SERIKALI YA TANZANIA YAWASILISHA MABORESHO YA MAENDELEO KATIKA MIKUTANO YA KIPUPWE INAYOENDELEA WASHINGTON DC

Ujumbe wa Tanzania kuwasilisha mpango wa maboresho ya maendeleo kwa Benki ya Dunia. Mpango huo unahusu maendeo katika  maeneo ya Elimu, Maji, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo na Usafirishaji

 Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Silvacius Likwelile pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dk. Philip Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho katika Elimu, Maji, Nishati, Usafirishaji, Rasilimali Fedha na Kilimo.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (katikati )akifafanua jambo wakati wa majadiliano, kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi, Philippe Dongier.

  

 Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akifafanua jambo katika majadiliano hayo.


Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Dk. Mpango akijibu hoja  baada ya kuwasilisha mpango wa maboresho. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha DK. Silvacius Likwelile na Kaimu Balozi  Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka.

No comments:

Post a Comment