Mikutano ya kipupwe imeanza rasmi mjini
Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi
ya 188. Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Augustiao William Mgimwa ni Gavana mmoja wapo
katika mikutano hiyo na Nchi ya Tanzania ni mwanachama katika mikutano hii.
Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe
maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya
kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana
mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la
Fedha la kimataifa pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya
kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Aidha pamoja na
mikutano hiyo kunakuwa na semina na majadiliano mbalimbali, mikutano ya
waandishi wa habari na matukio mbalimbali yanayohusu uchumi jumla , maendeleo
ya kimataifa na masoko ya kifedha ya kimataifa.
Mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa
na Magavana wa Benki itakuwa kipindi kijacho baada ya mikutano hii.
Bodi ya Magavana wa
Benki ya Dunia na Bodi ya Magavana wa
Shirika la Fedha la Kimataifa kwa
kawaida wanakutana mara moja kwa mwaka
kujadili kazi zinazohusu taasisi
zao. Mikutano ya mwaka ,
inayofanyika mwezi Septemba /
Oktoba huwa inafanyika mjini Washington
DC kwa miaka miwili mfululizo na mwaka wa tatu huwa inafanyika kwa nchi mwanachama.
Uzinduzi wa Mikutano hii
ya Bodi ya Magavana ilifanyika Sanannah, Georgia, USA mwezi March mwaka 1946.
Mkutano wa kwanza wa mwaka ulifanyika mjini Washington DC mwaka 1946.
Katika mikutano hiyo
ya mwaka makundi ambayo ni kamati za fedha, kamati za maendeleo, Nchi za kundi la kumi, Nchi za kundi la ishirini na nne na makundi
mbalimbali ya nchi wanachama wanafanya majumuisho ya mikutano hiyo na kila kundi linawasilisha makubaliano yao
katika mkutano mkuu wa mwaka. Mikutano ya mwaka inakuwa na utangulizi wa
mkutano wa siku moja ambapo Bodi ya Magavana wanafanya maamuzi ya namna mambo
ya sasa ya Shirika la Fedha la Kimataifa yanatambulika na kupitisha maazimio
husika.
Katika Mikutano hiyo ya
mwaka, mwenyekiti wake anakuwa Gavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la
Kimataifa, na uenyekiti huo ni wa mzunguko kati ya nchi wanachama kila mwaka.
Kila baada ya miaka miwili wanachagua Wakurugenzi watendaji. Kila mwaka wanakaribisha
wanachama wapya kuingia katika shirika la fedha la kimataifa na Benki ya Dunia.
Kwakuwa mikutano ya
mwaka inakusanya namba kubwa ya nchi wanachama wanaotambulika rasmi kwa pamoja, wanatoa nafasi ya ushauri mkubwa na mdogo, uliorasmi na usio rasmi.
Semina mbalimbali zinafanyika sanjari na mikutano hiyo, ikiwahusisha waendesha semina
kwa wanachama ambao ni wafanyakazi na waandishi wa habari. Mikutano ya mwaka imeweka semina ambazo
zitalenga katika makongamano ambayo yanajenga na yanahusisha sekta binafsi,
wawakilishi kutoka serikalini na maofisa wakuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa
na wafanyakazi wa Benki ya Dunia. Somo la fedha
za kimataifa ambalo kila mwaka
linatolewa kwa na Per Jacobsson kwa ufadhili wa Taasisi
iliyoanzishwa kwa heshima ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, pia inatolewa kila mwaka sambamba na mikutano
hiyo.
Mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha
la Kimataifa na Benki ya Dunia iliyofanyika nje ya Washington DC kuanzia mwaka 1947—2012
|
|
Mwaka
|
Mahali
|
1947
|
London
|
1950
|
Paris
|
1952
|
Mexico
City
|
1955
|
Istanbul
|
1958
|
New
Delhi
|
1961
|
Vienna
|
1964
|
Tokyo
|
1967
|
Rio
de Janeiro
|
1970
|
Copenhagen
|
1973
|
Nairobi
|
1976
|
Manila
|
1979
|
Belgrade
|
1982
|
Toronto
|
1985
|
Seoul
|
1988
|
Berlin
|
1991
|
Bangkok
|
1994
|
Madrid
|
1997
|
Hong
Kong
|
2000
|
Prague
|
2003
|
Dubai
|
2006
|
Singapore
|
2009
|
Istanbul
|
2012
|
Tokyo
|
Baadhi
ya Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao.
Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti, Monica Mwamunyange, Mhasibu Mkuu wa
Serikali, Mwanaidi Mtanda pamoja na Kamishna wa Sera, Beda Shallanda.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu
akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe.
Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha
Wajumbe
wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo pichani,
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dr. Joseph
Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor
pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip
Mpango.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu
akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe.
Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Harry Kitilya,
akitoa ufafanuzi katika kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania
kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana ,
Msafiri Nampesya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani , Suleiman Saleh wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu
masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw. Paul
Mwafongo.
Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na
Bi. Eva Valerian – Washington DC
No comments:
Post a Comment