Na Gladness Mushi,Arusha Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imezitaka nchi wanachama za maziwa makuu kujidhatiti zaidi ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa wanawake na watoto ili kutokomeza tatizo hilo ambalo ni kubwa miongoni mwa nchi hizo. Makamu wa rais, Dakta Mohamed Gharib Bilali amesema hayo leo mjini Arusha, alipokuwa akifungua mkutano wa mawaziri kutoka nchi 11 , wanaoshughulika na maswala ya wanawake na jinsia wa maziwa makuu ambapo amelitaja tatizo la ukatili wa wanawake na watoto kuwa ni kubwa sabna na linatishia usitawi na maendeleo ya jamii. Amesema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia ni kubwa hasa katika mataifa ya maziwa makuu kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea ikiwemo vita vinavyosababisha wanawake kufanyiwa vitendo vya ubakaji na ukatili mwingine huku wakiwa hawana mtetezi. Ameongeza kuwa takwimu zinaonesha kwamba pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa kukabiliana na tatizo la ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika nchi wanachama lakini bado tatizo la ukatili wa kinjisia na udhalilishaji ni kubwa sana ambapo ndani ya Nchi ya Tanzania kesi zinazohusu ukatili huo zimeongezeka kutoka 82,707 kwa mwaka 2002 hadi kufikia 88,527 kwa kipindi cha mwaka 2010. Kwa upande wake katibu mtendaji wa Sekretarieti ya nchi za maziwa makuu, balozi Liberata Mula mula, amesema mkutano huo ni wa kipekee kufanyika hapa nchini na umekuwa na mafanikio makubwa Amesema kuwa Sekretarieti hiyo imepokea taarifa ya utafiti wa kitaalamu uliofanywa katika nchi mbalimbali wanachama kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji yaliyotokea nchini Rwanda, wakati wa mauaji ya kimbari,na kufuatiwa na vitendo vya ubakaji Amesema kuwa makamu wa rais, Dakta Bilali, ametoa mwongozo ,na Tanzania imeshafanya mengi kuliko nchi zingine kuhusu ukomeshaji wa ukatili wa kijinsia na sasa kilichopo ni mkakati wa utekelezaji ndio changamoto kubwa inayoikabili Sekrtetariet hiyo. |
No comments:
Post a Comment