MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Saturday, November 5, 2011

SHEREHE ZA KUMPONGEZA RAIS WA ZANZIBAR DR SHEIN

Mwimbaji Sada Nassor wa Kikundi cha Zanzibar One,akiimba wimbo wa "Nidhibiti" wakati wa sherehe za CCM Zanzibar za kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuiongoza Zanzibar, huko katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,Salama Bwawani,wakati wa kumpongeza kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kwake kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar. PICHA NA RAMADHAN OTHMAN WA IKULU ZANZ
Kikundi cha Culture Musical Club,kikitumbuiza kwa nyimbo mbali mbali wakati wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar,huko ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar juzi.(3/11/2011).

No comments:

Post a Comment