MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Monday, June 25, 2012

Bungeni Dodoma waziri Mkuu, Mizengo Pinda asoma Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisoma Hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2012/13 Bungeni mjini Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akionyesha mikono yake juu kuonyesha kwamba yu mzima tofauti na taarifa zilizozagaa mwishoni mwa wiki kwamba alifumaniwa na kukatwa na mapanga mkoani Singida, amesema huo ni uzushi tu juu yake
Baadhi ya wabunge wakiwahi kikao cha Bunge



Mbunge wa Lindi Mjini(CUF) Salum Khalfan Barwany, (katikati) akiwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Tunu Pinda na Mtoto analelewa na Waziri Mkuu, George Bush nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma


Spika wa Bunge, Anne Makinda ampongeza Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla kwa kujibu maswali Bungeni kwa ufasaha ikiwa ni mara ya kwanza tangu ateuliwe katika wadhifa huo hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.
Naibu Waziri, Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala akipongezwa na Mbunge wa viti maalum Rita Mlaki baada ya kujibu kwa ufasha swali Bungeni aliloulizwa kuhusu wanariadha wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya  Michezo ya Olympic

Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala akijibu swali Bungeni mjini Dodoma jana

No comments:

Post a Comment