Monday, July 9, 2012
Rais Kikwete amkabidhi mama Maria Nyerere Tuzo ya Heshima ya Taifa la Burundi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mama Maria
Nyerere Tuzo ya Juu ya Heshima ya Taifa la Burundi aliyotunukiwa Baba wa Taifa
hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa
Burundi yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.Mwalimu Nyerere
alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa
Burundi ambapo alikuwa mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa nchi hiyo Prince Louis
Rwagasore. Rais Kikwete alimkabidhi Mama Maria tuzo hiyo leo asubuhi ikulu
jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment