Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi
ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa akimfariji paroko wa parokia ya Isimani, Angelo
Burgeo (60) na msaidizi
wake Herman Myalla (36) waliolazwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
kwa matitabu zaidi baada ya kuvamiwa na majambazi juzi na kuporwa
fedha zaidi ya shilingi Milioni 3.8( picha na Blog ya Francis Godwin)
Rais Dkt Jakaya Kikwete
amfariji paroko Angelo
Burgeo (60) na msaidizi
wake Herman Myalla (36) waliojeruhiwa na majambazi huku akiziomba
taasisi za dini kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha
ulinzi katika maeneo yao kama njia ya kukomesha matukio ya ujambazi
yanayofanyika katika maeneo ya taasisi za dini.
Rais Dkt Kikwete alitoa wito huo kupitia waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa ambako paroko huyo na mwenzake walivamiwa ,alitoa wito huo jana katika hospitali ya mkoa wa Iringa alipokuwa akiwasilisha salamu za Rais Jakaya Kikwete na kutoa pole kwa Paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa.
Novemba
15, mwaka huu mapadri hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa
wakiendelea na matibabu, walivamia na kushambuliwa kwa silaha za moto, mapanga
na nondo na majambazi.
Watu
watano wanaosikiliwa na polisi wakihusishwa na uhalifu huo katika tukio hilo
ambalo mapadri hao mbali na kujeruhiwa vibaya waliibiwa zaidi ya sh Milioni 3.8.
Akiwasilisha
salamu za Rais, Lukuvi alisema ametumwa kutoa pole kwa wahanga hao, waumini na viongozi
wa dhehebu hilo la dini kwa ujumla wake.
“Tupo
pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ambacho majambazi wamekuwa wakiwavamia
viongozi wa dhehebu hili la dini wakiamini mmehifadhi fedha na mali nyingine
nyingi ndani ya parokia zenu,” alisema.
Alisema
tukio la mapadri hao kuvamiwa na kujeruhiwa mkoani Iringa limekuja miezi
michache baada ya matukio kama hayo kutokea katika parokia za Migori na Pawaga
mkoani Iringa.
“Serikali
imefanya kazi ya kutoa mafunzo kwa mgambo wengi karibu katika kila kijiji, ni
wajibu wa taasisi hizi za dini kuwatumia hao au vinginevyo ikubali kushirikiana
na jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa walinzi wao,” alisema.
Akipokea
salamu hizo, Padro Burgeo alisema majambazi hao walifanikiwa kuingia ndani ya
parokia yake baada ya kutumia Mlango wa nyuma na kufanikiwa kuwapiga chenga
walinzi wao.
Alisema
katika tukio hilo ilikuwa afe lakini Mungu amesaidia kuyanusuru maisha yake
baada ya kufikishwa mikononi mwa madaktari.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Faustine Gwanchele alisema baada ya kumfanyia
upasuaji na kutoa risasi tatu kwa Padri Burgeo hali yake inaendelea vizuri
pamoja na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari
No comments:
Post a Comment