MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, November 22, 2012

Dk. Ali Mohamed Shein awasili Vietinam

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed  Shein,(katikati) akifuatana na mwenyeji wake Kiongozi Mkuu katika Ofisi ya Rais Ikulu Nchini Vietnam,Bw Giang Son,(wa pili kushoto) baada ya mapokezi rasmi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali,(kushoto) ni Balozi wa Tanzania Nchini China,pia akiwakilisha nchini Vietnam Philip Sang'ka Marmo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein,(katikati) akisalimiana na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini China,wanaoiwakilisha Tanzania Nchini Vietnam, wakati wa Mapokezi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam akiwa katika Ziara ya Kiserikali,pamoja na ujumbe wake aliofuatana nao,akiwemo Mama Mwanamwema Shein.Picha na Ramadhan Othman,Vietnam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein, akiteta jambo na  mwenyeji wake Kiongozi Mkuu katika Ofisi ya Rais Ikulu Nchini Vietnam Giang Son,wakiwa katika ukumbi wa Mapunziko  VIP  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali.Picha na Ramadhan Othman,Vietnam.
Mama Mwanamwema Shein,(kulia) Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman,(katikati) na Balozi wa Tanzania Nchini China,pia akiwa anafanya kazi zake nchini Vietnam, Philip Sang'ka Marmo,wakiwa katika Chumba cha Mapumziko  VIP  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam,wakiwa ni miongoni mwa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar Nchini Vietnam.Picha na Ramadhan Othman,Vietnam.

No comments:

Post a Comment