BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uganda (FUFA), limemteua Rais wa
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou, kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi
wa michuano ya kombe la Chalenji, itakayoanza Jumamosi, jijini Kampala, Uganda.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Afisa Habari wa
CECAFA, Rogers Mulindwa, tayari Hayotou, amekubali na atawasili Kampala,
akitokea Makao Makuu ya CAF, mjini Cairo, Misri.
Kiongozi huyo wa
mpira barani Afrika, anatarajiwa kuwasili jijini Kampala Novemba 22, ikiwa ni
moja ya malengo ya CECAFA ya kujiwekea mikakati imara ya maendeleo ya mpira wa
miguu katika Ukanda huo.
Hayatou amekubali
mwaliko huo, aliotumiwa na Rais wa CECAFA, Leodgar Tenga.
Kwa upande wake Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda
(FUFA), Lawrence Mulindwa, amesema Uganda inajivunia kuwa mwenyeji wa
mashindano hayo.
Katika msafara huo,
Hayatou, atafuatana na Maofisa mbalimbali wa CAF, akiwemo Katibu Mkuu, Hicham
El Amrani. Wengine watakaofuatana na Rais huyo wa CAF, ni Mohamed Raouraoua,
Constant Omari na Ngangue Appolinaire, ambapo mara baada ya kuwasili Kampala, Hayatou,
atakutana na viongozi wa ngazi za juu wa FUFA.
Akiwa nchini Uganda, Rais
huyo wa CAF, atahudhuria kikao cha Baraza la CECAFA, litakalofanyika Ijumaa
kwenye hoteli ya Serena, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, itakayofanyika
kwenye Uwanja wa Namboole.
Hayatou pia
atahudhuria sherehe iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake, katika Ukanda wa
CECAFA na Uganda
kwa ujumla.
Uganda
ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, watachuana na jirani zao, Kenya, katika
mechi ya ufunguzi Jumamosi
No comments:
Post a Comment