Ujumbe wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya MKUKUTA.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa
akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa. Benno Ndulu akijibu hoja kwa ujumbe wa
Benki ya Dunia huku Waziri wa Fedha Dk. Wiliam Mgimwa akimsikiliza
kwa makini.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Makhtar Diop aliyekaa
katikati, akitoa ufafanuzi wa mikakati wa vipaumbele hivyo. Kutoka
kushoto ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda
na Burundi Bw. Philippe Dongier na kulia ni Mkurugenzi wa Sekta ya
kupunguza umasikini na masuala ya Uchumi kanda ya Afrika Bw. Marcelo
Giugale.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini.
No comments:
Post a Comment