Moja ya miradi aliyotembelea na kuikagua, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, eneo la Mukuranga mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia wakazi wa Kijiji cha Mvuleni wilayani Mukuranga mkoani Pwani
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mvuleni kata ya Nyamto wilayni Mukuranga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, alipokuwa anahutubia
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akisalimiana na baadhi ya wazee wa Kijiji cha Mvuleni baada ya kuhutubia Mkutano wa hadhara kuhusiana na miradi ya Maji
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, amesema kwamba, Serikali inahakikisha miradi yote ya Maji inakamilika kwa wakati ili tatizo la Maji linalowakabili wananchi liweze kupungua kwa kiasi kikubwa
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mradi wa visma virefu eneo la Mukuranga mkoani Pwani, Makalla alisema matatizo haya ya Maji ambayo sasa wananchi wamechoka na ahadi za kila siku sasa Seriakli imeamua kufanya kwelli maana hakuna kitu kinachozuia kama ni fedha zipo za kutosha kilichobaki ni ushirikiano kati ya Kamati za Maji za maeneo husika na wakandarasi wa wilaya
Makalla alitembelea mradi wa Maji wa Nyamto uliopo kijiji cha Mvuleni ambapo mradi huo wa kisima kirefu umekamilika kwa asilimia 80 kilichobakia ni Pampu iliyoagizwa nchini Afrika Kusini na inatarajia kuwasili mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa nane na ikifika tayari uzalishaji wa Maji utakuwa umeanza ambao utahudumia vijiji takribani 13
No comments:
Post a Comment