MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, September 7, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAJI ACHANGIA SH MILIONI MBILI SHULE YA MSINGI MZUMBE

NAIBU Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Amos Makalla amechangia Sh milioni mbili kwa ajili ya kuweka Umeme katika Shule ya Msingiamewapongeza wazazi wa Kata ya Mzumbe kwa kujitolea katika michango mbalimbali ya maendelea ya shule.

Makalla aliyasema hayo, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Tangeni.
Alisema shule hiyo imekuwa na matokeo mazuri kwa kila mwaka kwa ushirikiano wa walimu na wazazi kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni.
"Nimefurahishwa na matokeo mazuri ya kila mwaka kwa shule hii, ushirikiano wa wazazi na walimu pia kufanikisha chakula kwa wanafunzi na ujenzi wa matundu 12 ya vyoo kwa mafanikio.
“Kwa kuwa mmeonesha uchu wa maendelea nami nawachangia Shilingi milioni mbili, kati ya hizo shilingi laki Tano zitumike kuingiza umeme na Shilingi milioni moja na nusu itumike kwa ajili ya kumalizia matundu 12 ya choo".alisema Makalla.
Pia alisema kwa sasa kazi iliyobaki ni kahakikisha kuwa  vyoo vinakamilika na wanafunzi wetu waanze kuvitumia.
Awali wakisoma risala kwa mgeni rasmi wahitimu hao katika risala yao, ilieleza changamoto ya upungufu nyumba za walimu na ukamilishaji matundu 12 ya choo na uingizaji umeme madarasa mawili.

Naye Diwani wa kata hiyo Theofila Jaka, akitoa shukrani kwa niaba ya walimu, wazazi na wanafunzi alimpongeza mbunge kwa kuhimiza maendelea katika kata hiyo.

“Mbunge makalla amekuwa kichocheo cha maendelea katika Kata ya Mzumbe nawaomba wananchi wa Tangeni katika uchanguzi ujao mchangueni Makalla ili muendelee kupata maendeleo,” alisema Jaka

Wanafunzi hao 45, wanatarajia kufanya mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi wiki hii

No comments:

Post a Comment